Hotuba ya JK May 2013

Bubu Msemaovyo

Platinum Member
Joined
May 9, 2007
Posts
4,189
Reaction score
3,552
Mh Rais Dr JMK Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda kuchukua fursa hii ambayo kwangu mimi ni nadra kuwa Mshauri wako lakini kwa wakati huu naomba nikupe ushauri huu mfupi ambao kwa mantiki una maana sana kwa lengo la kuhakikisha amani inarejea hapa nchini kama ilivyokuwa hapo awali.

Katika hotuba yako ya mwezi May nakusihi sana usisahau kukemea na wewe kama Rais toa kauli ya KUPIGA MARUFUKU MIHADHARA YA KIDINI. Midhara hii ipigwe marufuku kufanyika kokote iwe misikitini, makanisani au maeneo ya wazi. Kauli yao itakuwa imeungana na kauli waliyoitoa viongozi wa dini katika kikao chao kilichofanyika hivi karibuni hapa Dar es Salaam. Itakuwa ni rahisi kwako Mh kwasababu wenyewe tayari wameshaamua wewe huna wa kukulaumu cha msingi ni kupigilia msumali wa mwisho, hakika kufanya hivyo AMANI ITAREJEA TANZANIA na haitakuwa ni kisiwa cha amani tu bali Tanzania itakuwa ni BAHARI YA AMANI KILA MMOJA ATAPENDA KUOGELEA.

Sipendi kuwa na maneno mengi.

TANZANIA BILA MIHADHARA YA KIDINI INAWEZEKANA!!!​

Nawasilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…