KERO Hosteli ya Blue Pharmacy College of Health (Singida) si rafiki kwa Watoto, ipo karibu na danguro

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna Chuo kinaitwa Blue Pharmacy College of Health kipo Singida Mjini mbele ya Serengeti Pub kina hosteli za Wadada zipo opposite na Cheyo Lodge.

Concern yangu ni hizo hosteli zipo kwenye danguro la wadada wanaojiuza, yaani kuingia hapo hosteli nje ndo kuna Wadada wanaojiuza hiyo njia nzima (Cheyo Road).

Kiukwelii inaumiza sana yale mazingira siyo ya kuishi Watoto wa kike kabisa inawaathiri kisaikilojia sana na wengine wanajiingiza bila kutarajia. Wito wangu ihamishwe ile hosteli.
 
Back
Top Bottom