Hongereni wapinzani

Hongereni wapinzani

Comi

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2011
Posts
3,328
Reaction score
958
Kutokana na matokeo ya uchaguzi wa wiki iliyopita na haya ya marudio leo imejidhihirisha kuwa upinzani unakuwa kwa kasi. Matokeo hayo yawezakuwa ni matunda ya vyama hivyo kuungana(ukawa). Sasa jukumu lililombele ni viongozi waliochaguliwa kuonyesha kwa vitendo ili iwe rahisi katika uchaguzi ujao kupata viti vingi vya udiwani na ubunge.

Niwapongeze upinzani kwa kuendesha kampeni za amani ambazo zimeweza kuwapa elimu wananchi na kuweza kuchagua wale wanaowaamini kuwa wataweza kuwavusha katika miaka mitano. Pia niwapongeze viongozi kwa sababu pamoja na kutokea hujma za wazi,ukiukwaji wa utaratibu wa kupiga kura lakini bado wamekuwa na busara kwa kulinda amani ya nchi.

Hongereni viongozi wa chama tawala mnaopigania kuondoa amani ya nchi kwa ajili ya madaraka na maslahi yenu. ASIYEKUBALI KUSHINDWA SI MSHINDANI. Ni wakati wenu sasa wakujitathimini na kubadilika pale mnapoona mmelikosea taifa kabla ya uchaguzi mkuu mwakani. Mabavu mnayotumia sasa hivi ni msaada ambao mnawapa upinzani bure kwani wananchi watajiuliza hawa ccm wanataka nini kutoka kwetu hata watumie mabavu kiasi hiki.

Kwa matokeo yaliyokwisha toka ni dhahiri upinzani umepanda kwa kasi kubwa kwani ni nadharia ccm haijashinda bali imeshindwa kwani awali ilikuwa inamiliki hayo maeneo na sasa yameponyoka mikono mwake.

Hongereni upinzani kwa matokeo mazuri ila mnatakiwa kuendelea kutoa elimu ya uraia kwa wananchi kadri muwezavyo
 
Ile propoganda ya CCM, ukichagua upinzani vita itatokea,amani itavunjika imeishia wapi?
 
Ile propoganda ya ccm, ukichagua upinzani vita itatokea,amani itavunjika imeishia wapi?

Na ndio lilikua kimbilia la CCM kuwadanganya wananchi lakini wananchi sasa wamewashtukia hawataki tena ufisadi
 
Ccm bila ulaghai kushinda ni ngumu.

Kweli kabisa ndugu. Kama wanabisha hawajashindwa waseme wameongeza vijiji vingapi. Na hata hiyo asilimia wanayojivunia siyo sawa kwani wamedanganya sana. Ni sehemu nyingi tumeona kasoro za wasimamizi,kura kuzidi wapiga kura, wenyeviti kukimbia na masanduku ya kura. Je hayo yote yangefanywa na upinzani ccm ingekuwa na asilimia ngapi?
 
Back
Top Bottom