Hongereni FFU Arusha,huu ni mwanzo mzuri. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongereni FFU Arusha,huu ni mwanzo mzuri.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Oct 12, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tunaifahamu FFU,ndiyo na hata police tunawafahamu.FFU wanapashwa kutuliza fujo na police kulinda mali za wananchi,kutunza amani iliyopo na kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi kufuatana na maadili tuliyojiwekea katika jamii kama yapo.Hata hivyo nionayo yakifanywa na vyombo hivi ni kinyume kabisa na matarajio yangu.Vyombo hivi vimekuwa vikitetea na kulinda zaidi maslahi ya 'status quo' kuliko ya wananchi.Yale majukumu yao ya msingi wameyaacha kabisa.Tumeshuhudi police wakishiriki katika kunyang'anya haki za msingi kabisa za wananchi wakishirikiana na mahakama.Na pia tumeshuhudia mara nyingi police wakishiriki katika kunyang'anya mali za wanachi, wao wenyewe moja kwa moja au kwa kushirikiana na majambazi.Haya yako wazi.Police wengi wametajirika kwa kupewa fedha na mitandao ya majambazi ili wafumbie macho uovu wao.Mtandao wa Traffic police na ma-boss wao kukusanya pesa barabarani unaeleweka.Sio siri tena kwamba unaweza kuishia jela kwa kubambikizwa kesi kwa kosa ambalo hata hukutenda.Sasa katika mazoea haya,sio rahisi kukubali hili la Arusha,FFU kuwapiga viongozi wa CCM Mkoa na Wilaya,mm,haliingii akilini.Viongozi hawa walikuwa wanafanya vitendo ambavyo ni kinyume cha maadili ya jamii yetu.Sasa kama hawa ndio viongozi wanaopashwa kutuletea maisha bora,nadhani tumeingizwa mkenge.Nasema hili ni dogo, lakini ni mwanzo mzuri,wa kuanza kuondokana na mawazo kwamba kuna 'the untouchables',watu ambao wako juu ya sheria.Hongereni FFU Arusha.
   
 2. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mwanzo mzuri kumchania mtu shati, wakati ingekuwa upinzania watu wanapoteza maisha na hata kupata ulemavu wa kudumu. Hii ni habari ya kutunga tu ama walivamiwa na wahuni wakitaka chochote kutoka kwao.

  Kumbuka yaliyotokea Znz, huko tarime, mwembechai, n. k hii ni janja ya kufunika yanayotokea Tarime siwafagiilii polisi hata kidogo
   
 3. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Unajua, tunaelewa hawa jamaa wana uovu mwingi, lakini ni vizuri kuwapongeza hata kwa hako kadogo.
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2008
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Huu ni ujanja wa CCM baada ya kuona wakaazi wa kata ya Sombetini wako tayari kukifanya kile wasichotarajia wakaamua kuchukua mamluki kutoka kata zote za Arusha mjini na kufanya maandamano haramu.Mikutano ya kampeni ya CCM ilisusiwa na wananchi kwa ujumla,Kata ya Sombetini ni miongoni mwaka Kata kubwa kwa maana ya kuwa na wapiga kura wengi.
  CCM wanajua wakipoteza tena Sombetini maana yake uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ubunge utaenda upinzani[TLP].Bwana F Mrema na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha mjini bwana J Kileo walimhonga aliyekuwa diwani wa TLP bwana Mawazo ajiuzulu ili waweze kuirejesha kata ya Sombetini.Kuna kila dalili mgombea udiwani kwa tiketi ya TLP atashinda,wana mkakati wa CCM wameamua kuanzisha fujo pengine kuandaa uwanja mzuri wa kuiba kura.CCM waliweza kumrubuni bwana Mawazo na aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya TLP bwana Lema lakini wameshindwa kuwarubuni wakaazi wote wa kata ya Sombetini na hii ndiyo chanzo cha fujo za CCM.Wapinzani tuko imara kulinda kura zetu kwa gharama yoyote.
   
 5. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  When will we learn,that was for public consumption.FFU wakuchanie SHATI tu? hawa nao wajua mimi? nilipigwa magumi na mateke kwa eti kuwachomekea barabarani na nilipokwenda polisi walikataa kufungua jalada.
   
Loading...