Hongereni CRDB Kuchangia Ujenzi Polisi, Lakini Lazima Mchunguzwe kuhusu Malipo ya Bandari

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,307
4,585
BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA MILIONI 255 KWA AJILI YA KUSAIDIA UJENZI WA KITUO CHA KISASA CHA MAWASILIANO YA JESHI LA POLISI.




Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu (katikati), akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shs. milioni 255 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kituo cha mawasilianio ya Jeshi la Polisi. Kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna, Simon Siro, Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi, Omary Issa (wa pili kulia) na kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka.
(Picha na Francis Dande)

Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.

Baadhi ya wageni waalikwa.

Na Glory Chacky.

BENKI ya CRDB imekabidhi msaada wa sh. Milioni 255 kwa Jeshi la polisi kwa ajili yaujenzi wa kituo cha mawasiliano.

Akizungumza jana jijini Dar es salaam wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei amesema kuwa wanatambua kuwa jeshi la polisi ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi linahitaji mfumo bora wa mawasiliano kati yake na raia. Alisema wameamua kuelekeza msada huo kwa jeshi la polisi kwa kutambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na jeshi hilo ya kuhakusha kwamba kuna usalama na amani kwa raia.

Kimei alisema juhudi za wanachi katika kujikwamuakatika umaskinihazitafanikiwa kama kutakuwa na ukosefu wa usalama wa raia na mali zao kwa ujumla.

Naye mkuu wa Jeshi la polisi IGP, Ernest Mangu alisemakuwa wanashukuru kwa msaada huo kwani itasaudia kupunguza matukio ya kiualifu. “ Kituo hiki kitasaidia kulisogeza jeshi la polisi karibu zaidi na wananchi na kushirikiana nao katika kutaarifiana juu ya maswala ya kiualifu pindi yanapojitokeza”alisema Mangu.

Source: Michuzi Blog
 
Kwa hekima kidogo nilionayo naishauri management ya benki yetu tuhumiwa kulimaliza suala hili kwa kuilipa TPA tozo zote zinazotuhumiwa kupotea ama kuibwa katika mikono yake {kwa ushirikiano baina ya wafanyakazi wa CRDB na TPA} na pia kuwachukulia hatua kali za kinidhamu na kisheria wafanyakazi wote waliobainika kuiletea aibu na kutishia kuharibu sifa nzuri mbele ya jamii,wateja na wadau kwa vitendo vyao wafanyakazi wachache visivyo vya maadiri,miiko ya kazi .

Madhara ya malumbano ya nani kaiba,nani kaibiwa ,kaibiwa wapi,ushahidi wa kuibiwa au kuiba vitazidi kuivua nguo benki na kuwapa nguvu/faida washindani kibiashara hivyo kupoteza mapato,faida na magawio kufifia..Tatizo limalizwe kimya kimya kwa hekima na busara.
 
wengi hawajui kilichotokea TPA na kwingineko. wanasema kwa hasira na ghadhabu, na kisasi na wivu. wengi wao ni wasio nacho!
 
Back
Top Bottom