Hongereni CCM kwa kuonesha kujali Kalenga!

Hongereni CCM kwa kuonesha kujali Kalenga!

habariyamujini

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2013
Posts
3,094
Reaction score
457
MWIGULU NCHEMBA ,MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KALENGA WASHIRIKI MAZISHI YA WANANCHI WATATU KIJIJI CHA KIDAMALI MKOANI IRINGA

Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba na akishiriki mazishi ya wananchi watatu waliofarika kwa ajali ya gari,mazishi hayo yamefanyika jioni ya leo katika kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi mkoani humo.

Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga,mkoani Iringa,Ndugu Godfrey Mgimwa akishiriki mazishi ya wananchi watatu waliofarika kwa ajali ya gari,mazishi hayo yamefanyika jioni ya leo katika kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi mkoani humo.


Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Kidamali wakishiriki kwenye mazishi ya wananchi watatu waliofariki kwa ajali ya gari,iliotokea jana,mazishi hayo yamefanyika jioni ya leo ambapo.Katika mazishi hayo wanachama wa Chama cha CHADEMA na CCM walishiriki na kutoa ubani wao kwa wafiwa,ambapo CCM walitoa kiasi cha shilingi Miloni moja na CHADEMA shilingi Elfu Hamsini.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba na Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga,mkoani Iringa,Ndugu Godfrey Mgimwa wakiteta jambo kabla ya kwenda kutoa pole na kushiriki mazishi ya Wananchi watatu wa kijiji cha Kidamali,waliofariki kwa ajali ya gari hapo jana mkoani humo.

Source: Michuzi blog
 
Siasa za ajabu mtaacha lini. Ndugu yangu mmoja anasema wanapita ccm usiku nyumba kwa nyumba na kuwapa kila familia elfu kumi ili wawapigie kura
Ndugu zangu ccm acheni ulaghai wa kijinga mjue njia zenu zinajulikana kabisa
 
du! we nomama. swali 1) hizo rambi rambi, zilitolewa kwa kuhesabiwa kama sadaka za mafarisayo kipindi cha YESU?. (2) kama sivyo umezijuaje idadi yake?,
 
Back
Top Bottom