Hongera Waziri Mbarawa kwa "kudhibiti" ujanja ujanja Swissport, fitna zilizidi na kuondoa ushindani

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Hawa Swissport walibweteka sana,hawakuwa na mshindani ndani ya uwanja,yaani ilikuwa ni "One Man Show".

Hii Swissport ilikuja baada ya DAHACO(Dsm Handling Company) kubinafsishwa.Hii DAHACO ndio ilikuwa kampuni tanzu ya ATC.Kama ilivyo Swissport kampuni tanzu ya SwissAir.

Baada ya kubinafsishwa enzi za Mkapa,akapewa mtu mmoja anaitwa Gaudence Temu kama CEO baada ya mzungu aliyeibinafsisha kuondoka kurudi Makao makuu Zurich. Walipomuachia Temu hao wazungu ndio hali ikaharibika. Ikawa kama kampuni ya mfukoni. Mali kadhaa zilizokuwa za DAHACO zikaenda Swissport kwa mazingira ya ajabu ajabu.

Ground Handling Equipments kama "towing cars" (Schopf) kwa ajili ya kusukumia ndege kubwa vikabebwa na Swissport toka DAHACO, na ATCL akaingia gharama kubwa sana ya kuvikodisha vifaa ambavyo mwanzoni vilikuwa sehemu ya mbia wake. Huu ulikuwa ni mmoja kati ya ubinafsishaji wa hovyo hovyo kidogo.

Wizi wa mizigo, huduma mbovu, mishahara ya hovyo na asilimia ya ATC ndani ya Swissport iliyotokana na kubinafsishwa kwa DAHACO sijui iliishia wapi. Huyu bwana akafanya "ujanja ujanja" sana, kwanza wafanyakazi waliokuwa DAHACO walipelekwa Swissport bila kulipwa mafao yao ya kuitumikia DAHACO. Na huko Swissport wakaanza "upya"

Kila kampuni iliyokuwa inataka kuja Dsm kufanya huduma ya Passengers and Cargo Handling ilikutana na kikwazo cha Swissport. Akakosa mshindani na kubaki anabweteka. Yaani iwe kama vile TTCL bila Tigo au Airtel au Coca bila Pepsi, Simba bila Yanga na CCM bila Upinzani.

Kwa hiyo kwa kukosa upinzani huduma ikawa mbovu sana. Na kumbuka taswira ya kiwanja kimataifa inategemea na Ground Handling iliyopo. Swissport Tanzania ikawa hovyo sana sana. Inasemwa na ukabila na upendeleo vilitamalaki.

Huyu CEO wa Swissport miaka ya nyuma alikuwa anacheza na Waziri wa Wizara husika na kamati ya bunge ya miundombinu. Ikija tu kampuni mpya basi itawekewa vikwazo mpaka inaondoka. Inasadikika kamati ilikuwa inakula cha juu na inaiwekea vikwazo na waziri hatoi leseni. Hivyo Swissport kuendelea kufanya huduma bila mshindani.

Ilikuja kampuni moja kubwa sana ya Wasomali wa Uingereza inaitwa AFS...ikajenga na jengo kubwa sana kwa ajili ya kuanza Ground handling, cha ajabu Mamlaka ya Viwanja vya ndege wakatoa kibali kwa Swissport kwenda kujenga jengo lao mbele ya jengo la AFs. Hawa AFS mpaka leo hawana kazi ya maana sbb ya fitna za Temu na Swissport Tanzania.

Ikaja kampuni ya Equity Aviation toka South Africa, walichokutana nacho wanakijua wenyewe. Kwa hiyo huyu bwana wa Swissport akawa anajua njia za kupita na kuwablock wenzake na yeye kubaki kuwa "mtawala". Huwezi kuwa na uwanja mkubwa kama Julius Nyerere halafu mkawa na kampuni moja tu yenye vifaa vya maana vya kutoa huduma ya "Ground Handling"

Sasa kaingia JPM Mzee wa kunyoosha kama rula.Kampuni ya NAS toka Kuwait imeshinda vigezo vya kufanya kazi JNIA. Hii ni moja ya kampuni kubwa sana duniani kwa mambo ya handling(Google). Nchi nyingi kampuni hii inatoa huduma ya mafuta kwa ndege(JET A1) na AVGas(kwa sababu wanamiliki visima vya mafuta Kuwait), huduma ya "Sky Chefs" n.k; Kifupi sio kampuni lelemama

NAS ndio kampuni mojawapo ya muarabu ambayo inafanya Ground Handling pale Heathrow Inter'nal Airport. Yaani Muingereza na British Airways yake ndani ya ardhi yake anafanyiwa kazi na NAS na si kampuni za Waingereza. Emirates pale Dubai,na ndege nyingi za Kiarabu katka maeneo mengine nje ya nchi zao NAS ndio kampuni ya chaguo lao.

Hapa Tanzania hawa NAS Dar Airco wameungana na kampuni ya kitanzania inaitwa AIRCO iliyokuwa inafanya Ground Handling kule Mwanza. Ndio maana hii inaitwa NAS Dar Airco.

Hawa Swissport ndio walichangia kuiuwa hata ATC. Wanaojua "siasa za Aviation" wanaelewa. Sasa unapokuja kumlaumu Prof Mbarawa kwa kuipiga mkwara Swissport lazima ujue hata nyuma ya pazia kidogo. Maana hii Swissport inamfanyia sana fitna huyu NAS kwa kuchelewa kumuachia jengo ili aanze kazi zake. Na huyu CEO wa zamani inasadikika alipenyeza rupia kwenye kamati ya bunge zikawa za moto.

Hizi kamati za bunge na wajumbe wake huwa ni "deal". Ndio maana ukisikia mtu kapelekwa kwenye kamati ya Habari, Michezo na Utamaduni anatoa macho sana, maana huku huwezi kukuta Mmiliki wa Ndanda Fc anakukatia mkwanja wowote. Hana maslahi yoyote ya kutetewa bungeni.

Lakini ukiwa kamati ya miundombinu,basi lazima CEO wa TANROADS awatafute kwa chai, DG wa TAA akutafute kwa lunch ili uwanja uliojengwa chini ya kiwango usipigiwe kelele bungeni. Kule kamati ya Nishati lazima TANESCO wakuone kwa hela ya vocha, Migodi iwaangalie kwa tips ya vitafunwa. Ukiwa kwenye kamati ya POAC basi jua NSSF watakupa apartment kwenye moja ya majengo yao ukae bure ili lolote wanalosemwa bungeni uwakingie kifua.

Sasa ubunge sio "deal" sana. Mianya imekazwa,zile rupia zilizorushwa kwenye wale wa miundombinu ili kutetea kampuni aina ya Swissport zimegonga mwamba. Kuna mambo tunaweza tusikubaliane na Rais JPM, lakini kuna mambo lazima tukiri kuwa Mzee kanyoosha. Kila jema lina ubaya wake na kila baya halikosi hata jema dogo.

Ndio maana kama mnakumbuka,siku chache zilizopita huyu CEO Temu aliachia ngazi na nafasi hiyo kuchukuliwa na jamaa anaitwa Mrisho. Alishaona "zigo la kimba" litamuangukia. Na njia zake za ujanja ujanja za kuzuia kampuni nyingine kupitia kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu ziligundulika. Si ajabu hata kubadilishwa kwa wajumbe wa kamati na mwenyekiti wa kamati kupelekwa kwenye kamati isiyo na "deal" ya "kufungia magazeti" na "miswaada ya habari" ilitokea.

Kuna mengi sana juu ya hii Swissport na kauli ya Prof Mbarawa. Mengine tunayahifadhi. Binafsi bila unafiki na kwa kuzijua "siasa za usafiri wa anga" za Tanzania. Waziri kachelewa sana kuchukua hii hatua.

Kuna tamko la chama cha ACT Wazalendo liliwekwa humu na Mama Anna Mghwira juu ya mikakati ya kuifufua ATCL. Aliongolea sana juu ya suala hili. Hii ni hatua nzuri kuelekea kwenye maendeleo chanya kwenye usafiri wa anga Tanzania.

[HASHTAG]#bungelivekamamkutanoliveSimiyu[/HASHTAG] [HASHTAG]#LongLiveJF[/HASHTAG]
 
Umeandika mengi, inawezekana mengine yana ukweli na mengine ni simulizi ambazo hazijathibitishwa. Mimi hoja kuhusu ubinafsishwaji wa DAHACO.

1.DAHACO ilikuwa kampuni tanzu ya ATC ikabinafsishwa kwa Swissport. Je unapodai kwamba equipments zilichukuliwa kiujanja na Swissport una maana gani? Swiss-port hawakununua assets za DAHACO kwenye ubinafsishaji huo?

2. Kuhusu wafanyakazi waliokuwa DAHACO kwenda Swissport. Je Wafanyakazi hawakuwa na Chama chao kudai haki zao za kumalizika kwa mkataba ili walipwe? Au Swissport alinunua wafanyakzi wa DAHACO pamoja na haki zao zote?
 
barafu

Kama kawaida yako endelea kuihabarisha jamii ya Jamiiforums bila kuchoka kuhusu masuala ya usafiri wa anga nchini.

Nilishangaa sana kusoma baadhi ya komenti zikimlaumu Uamuzi Waziri Prof. Mbarawa lakini sikushangaa sana kwa sababu Tanzania inaugua ugonjwa wa siasa za fuata bendera.

Umepata ndondoo za kilicho nyuma ya moto katika uwanja wa JKNI?

Yes, Rais Magufuli ana mapungufu yake kama binadamu lakini ukiangalia kwa jicho la tatu lazima tu utampa pongezi kwa kazi anayoifanya kulingana na mazingira nchini.
 
Umeandika mengi, inawezekana mengine yana ukweli na mengine ni simulizi ambazo hazijathibitishwa. Mimi hoja kuhusu ubinafsishwaji wa DAHACO.

1.DAHACO ilikuwa kampuni tanzu ya ATC ikabinafsishwa kwa Swissport. Je unapodai kwamba equipments zilichukuliwa kiujanja na Swissport una maana gani? Swiss-port hawakununua assets za DAHACO kwenye ubinafsishaji huo?

2. Kuhusu wafanyakazi waliokuwa DAHACO kwenda Swissport. Je Wafanyakazi hawakuwa na Chama chao kudai haki zao za kumalizika kwa mkataba ili walipwe? Au Swissport alinunua wafanyakzi wa DAHACO pamoja na haki zao zote?
Mkuu hapa hoja sio ishu ya ubinafsishaji sijui na maslahi ya wafanyakazi wa DAHACO. Kama umemuelewa mtoa mada hiyo ni kibwagizo tu katika kutupatia picha/historia fupi kuhusu Swissport na walivyoanza kazi nchini Tanganyika,hayo yalishapita.

Hapa hoja ni jinsi hao Swissport wanavyohujumu na kuondoa ushindani wa kibiashara uwanja wa ndege wa Mwl. Nyerere na viwanja vingine.

Hebu rudia kusoma hoja ya mtoa mada mkuu.
 
Prof Mbarawa yupo sana kwenye twitter.

Infact, ni waziri pekee katika utawala wa Rais Magufuli anayepost twitter nyingi kuzidi mawaziri wengine.

Labda neno media lina maana nyingine.
Publicity matamko uchwara ndicho ninachomaanisha.....

Unaweza kuwa kwenye Twitter lakini your always talk fact na unaongea mambo positive huchokwi wala kuleta sintofahamu Kwa matamko yako....

Sio kama wakina Mwijage makonda wanavyokurupuka.........

Mfano ni makonda matamko ambayo ameshatoa na utekelezaji wake umeishia wapi?......
 
Umeandika mambo mengi sana Barafu na pia sijui yapi ni ya ukweli au yapi yametiwa chumvi.

Kuna picha ya mbali naiona una shida na Temu, hukuanza kumwongelea hapa.

Hivi ni kampuni gani duniani isiyofanya michezo ili iendelee kumiliki soko? Nini maana ya kwenda shule? Nini maana ya marketing strategies? Hao Nas nini sijui wameshindwa ku-penetrate kwenye market halafu mzigo abebeshwe Swissport?

Huko sijui kubinafishwa kwa DAHACO ni sera mbovu za Mkapa badala ya kuilaumu Swissport mlaumuni Mkapa.

Kwa mfano leo hii unakuja kumwondoa yule mama aliyepewa KIMAFA kwamba ndie mzigo wakati waliompa hilo eneo wapo wanagonga mvinyo?

Tafuteni njia ya ku settle matatizo ya kimfumo badala ya kukimbilia kuwatoa kafara baadhi ya watu au Mashirika

Halafu kwa maneno yako matamu sijui Nas inafanya handling Heathrow ni upofu tu kwani Swissport handling wanafanya KIA na JNIA pekee?

Swissport imechukua magari ya kusukumia ndege ya Dahaco kwani ubia wao ukoje? Hebu tusaidie nasi tujue kama ubia wa Swissport na Dahaco haukuhusisha kutumia vifaa vya Dahaco
 
Mungu amuongoze na amcmamie ktk shughul zk Profesa Muhongo kw kz nzur anayoifnya
 
Hongera kwa taarifa lakini tusisubiri janga la moto ndo tutoe hongera...!
 
Personally namkubali sana Professor Mbarawa. He is the man for the job!

Mkuu Barafu, jipu lingine ni ule mghahawa wa Flamingo..kwa kweli we need a new investor pale. Wale wahindi wamebweteka wanatoa huduma za hovyo..sehemu ni chafu ilmradi tuu. It is a joke.

I hope Prof. Mbarawa hatakubali wapewe ku-run restaurant kwenye Terminal Three ikifunguliwa. Ngoja nitafute email yake......nimwandikie. I am sure he may act on my views.

Halafu nasikitika sana. Sometimes unajiuliza hivi ile airport haina management? yaani vitu kama usafi, na vingine vidogo vidogo vinavyokera...mpaka waziri aingilie kati. Kama management team haiwezi kazi basi waondoke wengine wapewe kazi.

Thanks barafu kwa post zilizokwenda shule.
 
Bado hii mambo hamjamaliza?Si mngesema tuu kwamba ni ile kanda inayowasumbua kuanzia babu zenu ndio mpo tayari kuuza nchi ili muwatafute?
 
Back
Top Bottom