Msichokijua ni kua hili ni soko huria, serikali haifanyi biashara ila ni “regulator” kwa kutumia sheria taratibu na kanuni! Sasa la kuwapangia wenye magari mle wapi au hotel ziuzeje mnadhani ni rahisi?
Pia zile hotel zina varieties kutokana na purchasing power yako kama huwezi nyama choma ya 10,000 , nunua ndizi za kukaanga za mia tano na soda au kula matunda ya buku.
Mikoa ya kaskazini tumezoea haya mambo hata wa iringa na mbeya tangu enzi tumezoea pale Aljaazera!
Hata baadhi ya ndege walikua wana tabia ya kuuza viburudidho vingine ila sio abiria wote wana afford!
Kuna baadhi ya mambo ni jukumu la serikali ila mengine sasa tuwe tunatafuta ufumbuzi kama wateja/walaji, othetwise serikali za Kiafrica zitakua na mambo meeengi sana ya kufanya!
Huu ni mtazamo wangu tu!