Hongera Wambura mtani kwa kulisemea hili jukumu la wahusika kulifanyia kazi

Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
2,207
2,000
Moja ya vitu ambavyo ya vitu wana jf wamejaribu kulisemea hili la UUZWAJI WA VYAKULA KWA WASAFIRI HOTEL ZA BARABARANI ni wengi sana wamelipigia kelele sna lakn lilikosa backup ya vyombo vya habari hadi kuhisi pengine nao watu wa media wanachukua mlungula toka kwa wamiliki wa hizi hoteli ili lisipate nafas kuwafikia wahusika.

Lakini leo kupitia kipindi cha JE, HUU NI UUNGWANA? cha RADIO FREE AFRICA kinachoongozwa na mtangazaji WAMBURA MTANI amelisemea hili. Kiuweledi sana.

Kiukwel nawaomba hawa FCC TUME YA USHINDANI waingilie na hili wasitoe tu taaarifa za SIMBA TU wakumbuke na hili linawahusu pia

Bila kusahau chama cha kutetea walaji nacho huwa nakisikia tu ni wakati na wao kutoka watutetee jaman
 

kantalambaz

JF-Expert Member
Dec 24, 2017
1,740
2,000
Hao wanaotoa ushuhuda inaweza ikawa watu wa "kupangwa".tu wameambiwa cha kusema ili waumini tarajiwa washoboke zaidi. Kinachotafitwa hapo ni mpunga tu( sadaka ya pesa na mali nyingine zenye thamani) hakuna biashara ya kuponya au kusaidia waumini shida zao.

Hawa watu wa mabasi wanakera sana wanapeleka abiria kwenye hoteli zenye chakula kibovu alafu cha bei ghali hadi abiria wengine wanashindwa kumudu kupata chakula. Watu wa mabasi ni wabinafsi na wa imla hawajali kabisa abiria wao kwenye hili swala la chakula. Tuanahitaji kupaza sauti bila kukoma mpaka hili swala lipate ufumbuzi.
 

Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,599
2,000
Serikali ingeweka katazo la mabasi ya abiria kula kwenye hotel za njiani tofauti na stand.

Kwamfano njia ya Dar-Arusha stand ya Korogwe ni nusu ya safari,kujengwe ukumbi mkubwa na wakodishe vibanda vya chakula kwa raia za grade mbalimbali huduma zote zipatikane ndani.Serikali itapata mapato pia.

Hizo transit hotels zibaki kwa watumiaji wengine wa barabara
 

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
8,457
2,000
Serikali ingeweka katazo la mabasi ya abiria kula kwenye hotel za njiani tofauti na stand...
Shida iko hv katazo linatakiwa lije na solution, jambo ambalo ni impossible. Serikali bill ya umeme, maji, usafi etc kwa stand inawatoa jasho, sembuse kujenga ukumbi!!
 

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
4,412
2,000
Hao wanaotoa ushuhuda inaweza ikawa watu wa "kupangwa".tu wameambiwa cha kusema ili waumini tarajiwa washoboke zaidi. Kinachotafitwa hapo ni mpunga tu( sadaka ya pesa na mali nyingine zenye thamani) hakuna biashara ya kuponya au kusaidia waumini shida zao hawa watu wa mabasi wanakera sana wanapeleka abiria kwenye hoteli zenye chakula kibovu alafu cha bei ghali hadi abiria wengine wanashindwa kumudu kupata chakula. Watu wa mabasi ni wabinafsi na wa imla hawajali kabisa abiria wao kwenye hili swala la chakula. Tuanahitaji kupaza sauti bila kukoma mpaka hili swala lipate ufumbuzi.
Tumuombe mtangazaji wa star TV akomae nao kila jumapili kwa miezi mitatu bila kuchoka
 

Mwaikibaki

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,076
2,000
Msichokijua ni kua hili ni soko huria, serikali haifanyi biashara ila ni “regulator” kwa kutumia sheria taratibu na kanuni! Sasa la kuwapangia wenye magari mle wapi au hotel ziuzeje mnadhani ni rahisi?

Pia zile hotel zina varieties kutokana na purchasing power yako kama huwezi nyama choma ya 10,000 , nunua ndizi za kukaanga za mia tano na soda au kula matunda ya buku.

Mikoa ya kaskazini tumezoea haya mambo hata wa iringa na mbeya tangu enzi tumezoea pale Aljaazera!

Hata baadhi ya ndege walikua wana tabia ya kuuza viburudidho vingine ila sio abiria wote wana afford!

Kuna baadhi ya mambo ni jukumu la serikali ila mengine sasa tuwe tunatafuta ufumbuzi kama wateja/walaji, othetwise serikali za Kiafrica zitakua na mambo meeengi sana ya kufanya!

Huu ni mtazamo wangu tu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom