mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,666
Kila siku asubuhi katika kipindi cha KUMEPAMBAZUKA, Radio One FM huendesha kipindi ambacho mara nyingi hulenga kuibua kero za wananchi ambazo zingeweza kutatuliwa vyema na kwa haraka na watendaji wa Serikali na taasisi zake kama wangekuwa waadilifu na kufanya kazi jwa weledi.
Kipindi cha leo asubuhi kilihusu kupungua kwa bei ya mafuta ya magari/mitambo katika soko la dunia lakini hapa TZ bado bei haijashuka inavyotakiwa. Msemaji wa EWURA kajikanyaga kuuelezea hilo bila kuridhisha kiasi wasikilizaji wengi walimjibu na kuuliza maswali mengine kwa hasira. Hivi karibuni pia kulikuwa na kero kuhusu tozo la ushuru wa kwenye ankara za manununuzi ya umeme TANESCO, pia EWURA walijikanyaga.
Iko mifano mingi ya Taasisi nyingi za umma zilizoanzishwa ambazo badala ya kulinda haki ya mlaji na rasmali za umma zinamlinda mwejezaji na kuteketeza rasmali kwa faida ya waendeshaji.
Km DAWASCO wanatuma ankara za matumizi ya maji kwenye simu ya mteja bila kuanisha kiasi cha maji aliyotumia kwa muda huo wa mahesabu tofauti na ankara za maandishi ambazo silionesha "meter readings". Kwa hivi sasa hata "meter" za maji hazisomwi. Mlaji analipia hasara za uendeshaji na marupurupu ya viongozi.
Uendeshaji huu wa kifisadi ni wakati mwafaka wa kushughulikiwa.
CHUNGUZA CHAMBUA AMUA CHUKUA HATUA