Kwanza kabisa napenda kusema kwamba kitu nnacho post hapa binafsi hakinipi faida yoyote zaidi ya nchi yangu. Nampongeza Rais Magufuli kwa dhati ya moyo wangu kwa kurudisha mahusiano ya KIBALOZI na nchi ya ISRAEL. kwa kawaida sipendi kuandika mambo mengi, hivyo ntaenda kwenye point:
Jamani tutake tusitake mataifa haya mawili ISRAEL na SAUDI ARABIA , si mataifa ya kushindana nayo ubavu HATA SIKU MOJA. kwa sababu hiyo nampongeza sana rais na nasema wewe ni mwerevu. kuna mambo meeeengi ya kutolea mifano na maelezo ila kama nilivyosema sitaki kuwachosha hivyo ntatoa mifano michache.
Juzi juzi katika Ubalozi wa Saudia nchini Uturuki, amefariki muandishi wa habari wa Saudi arabia, niambie si marekani, si Urusi, uingereza Japan,china aliyelaani kile kitendo. Hata marekani amechagua maneno ya kusema, katika kuongelea suala hilo. lakini mnakumbuka jinsi Urusi ilivyotaka kumuua jasasi waka kwa sumu kule uingereza, hazikupita siku 3: vikwazo tayari.
Urusi inaendesha vita kule Syria, ilitaka kupeleka mitambo ya kisasa ya kutungua makombora S 400, Israel ilimwambia mrusi : nisije nikasikia hiyo kitu" mpaka leo hivyo mitambo haijapelekwa.
kuna mifano mingi na maelezo mengi sana, kwa kifupi haya mataifa , kiimani yanaheshimika sana, WEWE kama unapuuza naomba nikwambie MAREKANI baba yenu hoonigei hapo , sasa wewe ni nani mpaka ujifanye unavunja uhusiano na mataifa ambayo kiimani tunaamini ni mataifa matakatifu.
kuna siku nilileta thread hapa jamvini nikawaomba baadhi ya viongozi wa Dini ( nakumbuka nilimtaja Lusekelo,Gwajima na wengine) kuombea hiili suala,
mtu mmoja haraka sana ; akaandika 'scrap of the day'' sikumjibu , nilijua nnachofanya.
mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni ; kwa hili Magufuli nakupongeza sana, lakini pia mtazamo wa ujenzi wa viwanda pia mi nakupongeza sana. uko sahihi. huwezi kujenga nchi wote mnalima tu . naamini iko siku hata Mchuchuma haitakuwa hadith tena.