DOFFA
JF-Expert Member
- Jul 31, 2016
- 425
- 233
Chama cha Mapinduzi (CCM) kilizaliwa tarehe 5 ,Februari, 1977 kutokana na kuvunjwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP).Ni miaka 40 iliyopita sasa bila shaka ni umri wa mtu mzima aliyekomaa kifikra,kimienendo,kimtazamo na kimwili.
Pongezi kubwa ziwaendee uongozi wote wa chama kutoka juu mpaka kwenye mashina na matawi yake.
Hakika ccm ikiamua nchi itakwenda,M/kiti wake ni mwanasayansi mbobezi,katibu wake mkuu ni mtaalam wa mambo ya usalama,upande wa itikadi na uenezi kuna brain healer.
Matokeo yanaanza kuonekana hata kwa staili ya maadhimisho ya mwaka huu kwenye maeneo mbali mbali ndani na nje ya nchi.





Changamoto.
1.Wapo viongozi wanaoendeleza mazoea ndani ya chama hasa watendaji wa chama maeneo mbalimbali kwa kushindwa kuwa kiungo kati uongozi wa juu na wachini mf.maagizo kutoka juu kwenda kwa ngazi ya chini bado kuna cancer inasumbua.
2.Baadhi ya viongozi hawana uhalali wa kuendelea kuwa viongozi kwa kuendekeza maslahi binafsi.
3.Jumuiya kadha za chama maeneo mengi zime-paralyse kwa kuwa hazipati miongozo na taarifa sahihi kwa wakati kwenye maeneo yao.
4.Waliopewa dhamana kutanguliza mentality ya kuonekana kuwa wanafanya kazi sana lakini uhalisia hauko hivyo-danganya toto.
5.Ningependa sana uongozi uende kama kwa utafiti,uwazi,ubunifu,kuunganisha watu,hekima,busara nyingi kama wanavyofanya hawa viongozi wetu-samahani kwa kuwataja kwa vyeo vyenu.
MF.M/KITI NA MAKAMU WAKE,KATIBU MKUU NA KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI-HAKIKA KAZI YENU NI NZURI SANA.
****OMBI***Ondoeni uozo uliobaki-Wenyeviti na makatibu wengi ngazi za chini hawafanyi kazi inavyotakiwa.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.