Naona wale wa English academy mmeanza, siye wa yeboyebo tunatoka kapa. Tafadhali tufahamishe na siye, hapa ulitaka kusema nini?ha ha ha you will never full me let the leaders praise you
Originality kwa ZZK? Unatafuta mkojo wa kuku wewe! Waulize waliosoma naye pale UDSM watakuambia alivyokuwa mahiri wa "kudesa".
Originality kwa ZZK? Unatafuta mkojo wa kuku wewe! Waulize waliosoma naye pale UDSM watakuambia alivyokuwa mahiri wa "kudesa".
Katika siku za hivi karibuni Mh Zitto Kabwe mbunge wa Kigoma kasikazini(CHADEMA) amekuwa akiandika makala katika magazeti mbalimbali hususani magazeti ya RAIA MWEMA na TANZANIA DAIMA. Nampongeza kwa hilo ni dalili kuwa kiongozi huyu ana tabia ya kujisomea jambo ambalo halifanywi na watanzania wengi wakiwemo viongozi.
Katika makala zake mbili zilizotoka mfululizo katika gazeti la RAIA MWEMA toleo namba 278 na 279, Mh Zitto alichofanya ni kutuhabarisha kuhusu kazi zilizofanywa na kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma(POAC) ambayo yeye ni mwenyekiti wake. Sijawahi kuwa mbunge wala mtumishi wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania hivyo lazima nikiri sina uelewa wa kutosha wa shughuli za bunge na kamati zake. Lakini naelewa kuwa kila kamati ya bunge huwa na katibu/makatibu ambao ni watumishi wa bunge. Katibu wa kamati ana jukumu la kuandika minutes za vikao vya kamati kwaajili ya kumbukumbu za kibunge(hansard). Ninachojaribu kueleza hapa ni kuwa makala hizo za Mh Zitto si makala za ubunifu bali ni taarifa ambazo zingeweza kutolewa na katibu wa kamati au katibu wa bunge kwani ni matokeo ya vikao kati ya POAC na mashirika mbalimbali ya umma yaliyofanya vikao na kamati husika.
Mwanahabari Ezekiel Kamwaga hivi karibuni aliandika makala katika gazeti la RAIA MWEMA akimsifia Zitto kwa uandishi makala murua na kwamba hiyo ni sifa ya ziada kwa mtu anayetarajia kugombea urais. Sitaki kupingana na Kamwaga katika hilo ila ambacho naamnini Kamwaga hakukisema kwa makusudi ni kwamba makala hizo basi ziwe ni za mwandishi mwenyewe na si taarifa za kamati ambazo zinaweza kutolewa na mjumbe yoyote wa kamati au afisa habari wa bunge.
Sina lengo la kumvunja moyo mhe Zitto Kabwe bali nampongeza kwa kutenga muda kuandika makala pamoja na kuwa na shughuli nyingi ila namshauri ajitahidi kuandika makala zake mwenyewe na si kuturipotia kazi za kamati yake, hivyo Hon Zitto should strive for originality kama anataka kutembea/kuishi kwenye mitazamo ya rafiki yake Kamwaga juu ya uandishi/urais. NAWASILISHA
Mkuu mwakidondo kwanza nikupongeze kwa kufuatilia makala za ZZK kwa kuzisoma na kuzielewa na kuzichambua. Binafsi nilisoma makala zake kama mbili hivi, mojawpo ni ya Partice Lumumba. UKiangalia, style ya uandishi anayoitumia, ni kutoa historia ya kitu, na kwa mbaali katika kila historia yenye mguso wa kimaslahi ya kisiasa, kimapinduzi na kiuchumi anaiubua hoja kidogo, na kuiacha na kuendelea na historia nyingine katika jambo hilo.
Katiak kufuata stayle hii, anajaribu sana, kuvuta hisia za msomaji na kumfanya kwanaza ajue historia na kutambua ni nini kinaongelewa, kabla hajatoa hitimisho kulingana na dhamira yake katika makala hiyo.
Sijui kwa watalama wa insha/makala wanaitaje aina hii ya uandishi. Na ukisoma vizuri zaidi, Hitimisho lake huwa linajaribu kugusa kila eneo la historia aliloongelea na nini kinatakiwa kufanywa na watanzania, au wanasiasa ili kuweka mambo sawa. Mahitimisho yake, mimi binafsi nimekuwa nikiyapenda sana, na aina hii ya uandishi nimeupenda kwa kuwa unakupa nafasi ya kujua historia kwanza.
Kuhusu suala la POAC siwezi lisemea sana kwani sijasoma hiyo makala. Lakini kwa mtazamo wangu, anaweza akawa anatoa taarifa kama ile ile ambayo inatolewa na Bunge (inayotakiwa kutolewa na Bunge), lakini, Kikubwani kuangalia, Hitimisho lake ndo litabeba ujumbe mzito na wa maana, na si kuelezea weee na bila kunyambulisha dhima na dhana nzima ya hiyo makala aka ushauri. Ndo maana mkuu, hata hapa JF, unaweza uka copy na ku-paste story ya mtu na kuiweka hapa, lakini mwisho wa siku watu watakuuliza, what is your take??.
Mkuu, kuandika ni kazi kweli kweli, na ni talanta pia, wengine ukitupatia kalamu tuandike inakuwa tabu kidogo, kwa hiyo ushauri wako ni mzuri na jinsi ulivyoelezea nakupa big up mkuu mwakidondo, nadiriki kusema, kuna kitu nimejifunza hapa!