Babu wa Kambo
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 559
- 808
Kila mfuatiliaji mzuri wa Siasa za hapa Tanzania ataafikiana na mimi kwamba siku kadhaa hizi Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, amekuwa moto mkali sana hasa baada ya kuanza zile vuta nikuvute Bungeni Naibu Spika alipozuia mjadala wa Wanafunzi wa UDOM ambapo ilipelekea Wabunge kadhaa wa upinzani kufungiwa vikao vya Bunge akiwemo na Zitto mwenyewe
Nasema amekuwa moto kwa sababu Siasa anazozifanya sasa ni tofauti kabisa na aina ya Siasa zake tulizozoea kuziona, yeye huwa ni mtu wa mapambano ya hoja huku akikanyaga kwa tahadhari kubwa, lakini kwa sasa hata anavyoongea tu utagundua kabisa kuna kitu, unaona kabisa ni mtu aliyeamua "lolote na liwe", hakuna tahadhari tena, ni mtu aliyedhamiria. Hizi siyo Siasa za Zitto, japo kidogo alizijaribu akiwa na Chadema lakini si kwa kiwango hiki
Ukimtazama unagundua sasa ni mtu aliyeamua rasmi kupambana na "Mfumo" kandamizi, Mfumo wa Kidikteta chini ya chama kimoja, lakini je wengine tunajiuliza, Mfumo huo ndiyo kauona leo? Kila neno analotoa juu ya Mfumo unaliona ni la ukweli mtupu, lakini je huu ni wakati wake? Jibu ni hapana
Ukweli ni kwamba harakati zake hizi ziko nje ya wakati, it's too late. Utawala huu wa mabavu mnaoulalamikia leo mliuruhusu wenyewe
Unapotaka kupambana na Mfumo ni ngumu sana kuanza papo kwa papo na ukaushinda, wenzake waliliona hili, lakini yeye aliutumia vibaya muda wake akawageuka, haya ndiyo Matunda yake. Kipindi wanafanya yale mapambano ya kuundoa Mfumo-Dola uliojengwa na CCM kipindi yuko CHADEMA ule ndio ulikuwa muda muafaka na si sasa, kipindi kile Mfumo ulikuwa umedhoofu chini ya uongozi dhaifu wa JK ndicho kilikuwa kipindi cha kuuangusha lakini si sasa ambapo mtu mmoja mwenye nguvu amakuja kutengeneza wa kwake na unaomuogopa mno, ni ngumu kuuangusha kirahisi. Ili kuuangusha inabidi kuudhoofisha kwanza, hii haitakuwa kazi rahisi kama anavyodhani Zitto
Anayokula sasa ni "matunda ya usaliti", alidhani anaikomoa CHADEMA na viongozi wake, lakini sasa ndipo anajua kumbe aliisaliti nafsi yake na Taifa lake, ile ndiyo ilikuwa saa ya ukombozi, kwa sasa atapoteza muda na Rasilimali za chama chake bure. Najua anatamani sana apate support ya vyama vingine, kwa bahati mbaya hivyo vyama vingine ndivyo alivyovisaliti kwa mara nyingine kwa kuanzisha Siasa zisizofaa kipindi cha uchaguzi matokeo yake akaipa nguvu zaidi CCM na wateule wake, hakuutambua muda muafaka wa kuunganisha nguvu
Mwisho niseme, sisemi haya kumkatisha tamaa Zitto na Chama chake lakini wengine sisi hupenda kusema ukweli, harakati za Zitto, dhamira ya dhati ya Zitto, vimekuja kwa kuchelewa. Amemaua kupambana kwa sababu yanayomfika sasa ni yale aliyozoea kuyasikia kwa wenzake, ameonja uchungu wake, kusakwa na Polisi kusiko na utaratibu hakukuwahi kumwandama kama ilivyo sasa, ya kufukuzwa Bungeni kusiko na utaratibu yalikuwa ni mambo ya akina LEMA. Hakutaka kuwa mpinzani halisi katika wakati uliofaa
Kila la kheri Zitto na ACT, lakini mko nje ya wakati, poleni kwa mikikimiki mnayopitia, Mfumo huu hautaanguka bila kuudhoofisha kwanza, mapambano haya yanahitaji mtafute nguvu ya pamoja. Poleni wapinzani kwa ujumla wenu