Darkish
JF-Expert Member
- Sep 25, 2014
- 314
- 327
Hoja yangu ni kuzungumzia nyumba za ibada zisizo rasmi kwa maana ya makanisa na misikiti zinazoendelea kuchipuka ndani ya makazi ya watu hasa maeneo yasiyopimwa au kwa jina lingine makazi holela. Utakuta mtu binafsi ananunua makazi holela ya mtu mwingine yaani nyumba moja halafu anaanza kujenga nyumba ya ibada katikati ya nyumba zilizobanana hazina hata uchochoro wa kupitisha hata pikipiki.
Nje juu ya paa anatundika spika kubwa nne ambazo zinafunguliwa kwa sauti ya juu sana kiasi ambacho hata mtu aliye umbali wa kilomita zaidi ya moja anakosa amani kabisa na hasa kama anauguliwa. Nyumba hizi za ibada zimeongezeka sana katika eneo dogo la makazi ya watu kiasi ambacho unahisi labda wapo katika mashindano ya kugombea waumini au sadaka au misaada inayotolewa na wafadhili wao.
Spika zitaanza kuunguruma saa 10 alfajiri na wataendelea hivyo kila baada ya masaa mawili hadi saa 2 usiku. Wengine wataendelea kuhubiri na kuimba kwa sauti kubwa kuanzia usiku hadi alfajiri. Lakini kinachoshangaza sasa ni kuona nyumba hizi za ibada nyingine ni zimejigeuza kuwa taasisi za kielimu ya dini kwa kujenga mabweni na kukusanya vijana kutoka mikoani na kuwaleta Dar es Salaam na kuwaficha humo kwa kisingizio cha kuwapa elimu ya dini.
Nilijaribu kudadisi wanapata wapi uwezo wa kuwatunza hao vijana wote na jibu rahisi nililopewa ni kwamba wanafadhiliwa na misaada kutoka Saudi Arabia. Ninachoshangaa ni kwamba kama wanapata misaada mikubwa kiasi hicho kwa nini wasinunue maeneo rasmi yaliyopimwa na serikali, wakasajiri taasisi zao na wakapewa vibali vinavyotambulika kuliko kuja kujibana kwenye makazi ya watu holela, yasiopimwa, yaliokwishajaa na mabondeni.
Ukizungukia maeneo ya Vingunguti hasa katika bonde la mto Msimbazi kuelekea Karakata bondeni nyumba hizi za ibada zimeibuka sana na zinaendelea kujengwa kwa kasi, je wenzetu hawa wana vibali vya kuweka majengo haya ya kudumu mabondeni na je serikali inabariki mwenendo huu!!?
Mheshimiwa Makonda upo wapi, tafadhali nakuomba zungukia hata huku uswahilini kwetu, kero sio maji tu au madawa ya kulevya peke yake mengineyo yapo vilevile ila watu wanaogopa kuyaweka wazi haya mambo wakihofia kutupiwa sijui mapepo sijui majini.