Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,941
- 51,063
- Thread starter
-
- #21
Kama serikali inashindwa kudai deni la mtu mmoja mbowe basi ni dhaifu sana. Yaani mtu kulipa deni mpaka aambiwe na wengine wakati serikali inayomdai ipo.Majizi chadema mwambieni Mbowe alipe Deni la Nhc na pia alipe wafanyakazi wa gazeti la Tanzania daima.
Mwambieni aache maigizo ya kukata, funua na kushika ukuta
Kisheria na kimfumo Mwenyekiti wa kijiji ana "Serikali" lakini Diwani ni mwakilishi tu wa mawazo ya wenye serikali zao kwenye Halmashauri. Lakini kwa kuwa kwa muda mrefu Halmashauri nyingi zilikuwa chini ya CCM Madiwani walikuwa ni wajumbe wa Kamati za siasa za Kata kwa ivo kichama walikuwa na nguvu na ushawishi mkubwa sana kuliko wenyeviti wa vijiji ama mtaa. Matokeo yake Madiwani wakati mwingine hujifanya kuwa wao ni mabosi wa Wenyeviti wa mitaa/vijiji.Itapunguza gharama za uendeshaji,jiulize kama kuna mwenyekiti wa kijiji na mtendaji wa kijiji sio sababu ya kuwepo diwani.
Mirija imekatwa wapiga dealKwa sasa Halmashauri karibu zote ziko taabani. Hakuna fedha inayoshushwa kwa ajili ya miradi,other charges. Inafikia wakati hata hela ya kununua rimu moja ya karatasi wanakosa. Kwa kweli Serikali Kuu iwashushie fedha zao kama zilivyopangwa na kuidhinishwa kwenye bajeti.
Halmashauri ya rombo chini ya chadema tokea 1995 ndio inaongoza kwa rushwa nchini!!!
Yani kamaa mm nilifiwa na mtoto wangu halmashauli Ya Mkuranga walishindwa jlkuniudumia wakasema nizike tu watanirudishia gharama zangu lakini mwaka sasa unaisha kilanikifuatilia naambiwa Pesa hazijaletwa yanishida kwelikwelKwa sasa Halmashauri karibu zote ziko taabani. Hakuna fedha inayoshushwa kwa ajili ya miradi,other charges. Inafikia wakati hata hela ya kununua rimu moja ya karatasi wanakosa. Kwa kweli Serikali Kuu iwashushie fedha zao kama zilivyopangwa na kuidhinishwa kwenye bajeti.
Hela zilizoibwa kwa wingi nchi hii hazikuibwa kwenye ngazi ya Halmashauri bali kwa hao hao unaodhani wamekata mirija ya wenzao. Magufuli wakati akiwa waziri wa Ujenzi, wizara yake ilituhumiwa na CAG kufuja mabilioni ya shilingi ya wizara hiyo. EPA, Kagoda, Tangold,Meremereta, Escrow,IPTL,TTCL, na madudu mengi yaliyoifilisi hii nchi yetu hayakutokea kwenye ngazi za Halmashauri bali kwenye ngazi yao wapenda ugandamizaji wa Halmashauri.Mirija imekatwa wapiga deal