Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Polisi (kinyume na sheria inayosimamia mikutano ya hadhara), wamezuia mkutano wangu wa hadhara uliokuwa umepangwa na kuandaliwa kufanyika leo Wilaya ya Ilemela.
Hakuna sababu yoyote ya maana zaidi ya mwendelezo wa utawala unaokiuka sheria na kuvunja misingi ya demokrasia na hatimaye ustawi wa jamii.
...
Sababu nyingine ni hofu. Hii ni dalili ya kuwa utawala huu umejawa na hofu sana. Hofu kuanzia kwenye ukweli kuwa hawakushinda uchaguzi. The guilty are afraid.
Wana hofu na namna wanavyoendesha serikali. Hawajiamini. Wanajua kupitia mikutano hii wananchi wataambiwa ukweli kuhusu kukwama kwa bajeti hewa ya serikali, utawala wao unavyosababisha hali ngumu ya maisha kwa wananchi kwa mikakati mibovu ya kutekeleza sera za uchumi, utawala wao unavyokiuka haki za binadamu kwa kupuuza Katiba na Sheria za nchi.
Wana hofu kuwa kwenye mikutano hii wataumbuliwa namna ambavyo wanaipeleka nchi katika hali mbaya kwa kauli na matamko yanayotishia mstakabali wa nchi na umoja wa kitaifa.
Ukweli ni kwamba sababu zote alizotumia OCD huyo wa Ilemela si za msingi na sheria hampi kabisa mamlaka ya kuzuia mkutano wa hadhara bali amefanya hivyo kwa maelekezo aliyopewa baada ya kuuliza afanye nini!
Taarifa nilizonazo ni kwamba Mbunge wa Jimbo la Ilemela hana mkutano wowote leo jimboni kwake achilia mahali hapo palipotajwa. Lakini hata kama angekuwa nao ofisi yangu ilikuwa imeshabadili eneo la mkutano na kupeleka taarifa kwa DED na OCD kuwa tutatumia Uwanja wa Sabasaba.
OCD alipoamua kujibu hiyo barua (siku tatu baadae hali inayoonesha kuwa alikuwa anatafuta maelekezo kwanza), akajibu barua moja tu ya awali iliyokuwa inazungumzia Uwanja wa Stendi Pasiansi ambao tuliamua kuucha kwa sababu siku hizi umekuwa mdogo kutokana na ujenzi wa barabara unaoendelea barabara ya kwenda Airport.
Ofisi yangu ilipowasiliana naye kumweleza kuwa mbona kajibu barua moja tu ya zamani na kwamba pia hana mamlaka ya kuzuia mkutano bali ku-regulate kwa kufanya majadiliano kuhusu muda au mahali, akawa mkali akisema kuwa mkutano ukifanyika yeye atatumia PLAN B kuhakikisha haufanyiki.
Hiyo plan B anayoijua yeye, haikuweza kutumika kufanikisha mkutano?
Kwa hiyo, hofu haiko tu kwa mkubwa wao. Imeshuka hadi kwa baadhi ya wabunge wao. Hawajiamini. Wanajua hwakubaliki kwa wananchi. Wanadhani kuzuia sisi kukutana na wananchi kutawapatia ahueni wao.
Jitihada za ofisi ya Mbunge kuwasiliana na mamlaka zingine kuhakikisha mkutano huu uliopangwa kufanyika leo hadi sasa hazijafanikiwa kwa bahati mbaya maamuzi yanapaswa kufanywa na makada wa CCM walioko serikalini hapo mkoani.
Kwamba polisi wamefikia hatua hawana uwezo wa kusimamia sheria, weledi wa kazi yao kwa jambo ambalo liko ndani ya uwezo wao kisheria, hadi wapate maelekezo ya wanasiasa ni jambo la hatari sana katika kusimamia misingi ya haki nchini.