Hizza Tambwe, Lwakatare, Akwilombe waomba kurejea CUF

He!!! Au ni Alubadili?
 

Huyu Cuf ngangari ni mtatiro nini? Kweli Cuf mmeishiwa kwa kiwango hicho mpaka mnatamani kurudisha watu wa zamani.Jengeni chama achaneni na ndoa yenu na ccm,ETI CHADEMA WAANZE KUFIKIRIA KUMKARIBISHA TENA SHITAMBALA? Chama imara kinavutia watu makini wapya.
 

Kwa Lwakatare na Akwilombe sina cha kusema, lakini kwa huyu Tambwe ninayemfahamu nina shaka sana.
Tambwe Hizza hana jipya na ame-prove katika mijadala mingi ya kisiasa kuwa na uelewa mdogo katika
kupambanua na kuchambua mambo. Wananchi wa Jimbo la Temeke wanaelewa hilo na waliliona siku nyingi
ndiyo maana walimnyima fursa ya kuwaongoza.

Tambwe amewahi kugombea ubunge katika jimbo la Temeke mara sita na kubwagwa:
*Kwa mara ya kwanza aligombea kupitia NCCR-Mageuzi mwaka 1995 na kubwagwa
na Ramadhan Ali Kihiyo wa CCM.
*Mwaka 1996 aligombea tena kupitia Chama cha Wananchi (CUF) katika uchaguzi mdogo,
kufuatia kujiuzulu kwa Kihiyo kwa matatizo ya afya, lakini alibwagwa na Augustine Mrema (NCCR-Mageuzi).
*Tambwe aligombea tena kupitia CUF baada ya Augustine Mrema kutangaza kujiengua NCCR-Mageuzi
na kujiunga na Tanzania Labour ambapo kisheria alikuwa amepoteza wadhifa wake wa ubunge, hata hivyo
Tambwe alishindwa na John Kibaso wa CCM.
*Mwaka 2000 aligombea tena kupitia CUF akabwagwa na Hadija Kusaga wa CCM.
*Mwaka 2005 alijaribu tena kupitia CUF lakini akabwagwa na Abbas Mtemvu (CCM),
*na mwaka jana 2010 aligombea tena kupitia CCM lakini akabwagwa katika kura za maoni
na Mbunge wa sasa, Abbas Mtemvu.
 

umbea au? kama ni kweli bado hujawa qualified kwa umbea!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…