Hizi ni rekodi za soka ambazo ni ngumu kuzivunja na huenda huzijui.

Hizi ni rekodi za soka ambazo ni ngumu kuzivunja na huenda huzijui.

01 ◉ Edson Arantes jina la utani, Pele
ndiye binadamu anayeshikilia rekodi ya kufunga magoli mengi zaidi Duniani (1,281) including na magoli ya mechi za kirafiki.

02 ◉ Sergio Ramos anashikilia rekodi ya kuoneshwa kadi nyingi zaidi za njano (26) ndani ya mechi (38).

03 ◉ Kwenye top six EPL, Tottenham ndio klabu ambayo haijatwaa ubingwa wa ligi kuu kwa muda mrefu zaidi. Wana miaka (59) bila kutwaa kombe la ligi kuu.

04 ◉ Lionel Messi
ndiye binadamu pekee aliyefunga magoli mengi zaidi (91) ndani ya calendar ya mwaka mmoja.

» Messi pia ndiye binadamu pekee aliyetwaa tuzo nyingi zaidi za Ballon D'Or (7).

» Rais wa Liberia
, George Weah anashikilia rekodi ya kuwa mwafrika pekee aliyetwaa tuzo ya Ballon D'Or.

05 ◉ Robert Lewandowski
anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi (5) katika mechi moja ndani ya dakika chache (9').

06 ◉ Jesse Lingard anashikilia rekodi ya forward aliyecheza mechi nyingi (25) bila kupiga shuti lolote golini.

07◉ Eric Bailly
ndiye mchezaji pekee UEFA Champions league aliyepiga shuti mpira ukatoka nje ya stadium katika karne ya (21) ›› Man United vs Valencia.

08 ◉ Klabu ya Liverpool
󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 inashikilia rekodi ya Dunia ya kukusanya points nyingi (97) kwenye msimu mmoja wa ligi yenye timu (20) bila kutwaa Ubingwa wa ligi kuu (18/19).

09 ◉ Sadio Mane
anashikilia rekodi ya kufunga hat-trick ya mapema zaidi (Dakika 2') akiwa Southampton
󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿.

10 ◉ Real Madrid ni klabu pekee kwenye historia iliyotwaa Ubingwa wa UEFA champions league mara (3) mfululizo


11 ◉ Hary Kane amefunga magoli (155) bila kutwaa kombe lolote


12 ◉ Aaron Svesve anashikilia rekodi ya kucheza dakika 90' bila kugusa mpira !!

13 ◉ Egypt
ambao ni mabingwa mara (7) wa Africa hawajawahi kushinda mechi yoyote kwenye kombe la Dunia !!

14 ◉ Suleyman Mamam wa timu ya taifa ya Togo
alicheza soka dhidi ya Zambia
2001 akiwa na umri wa miaka 13 na siku (310).

15 ◉ Golikipa Tom King kutoka Wales
󠁧󠁢󠁷󠁬󠁳󠁿 anashikilia rekodi ya kufunga goli kwa umbali mrefu zaidi. 21 January 2021 aliifungia goli klabu yake ya Newport county akiwa kwenye (6), umbali wa (96.01) meters.

16 ◉ Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi zaidi ya kichwa Duniani (145).

17 ◉ Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi zaidi UEFA champions league (140) anashikilia pia rekodi ya kufunga magoli mengi zaidi kwenye timu za taifa Duniani (123).

18 ◉ Pele
alikuwa binadamu pekee aliyetwaa mara tatu kombe la Dunia. Rekodi hiyo inaishi mpaka sasa

19 ◉ Arsenal wanashikilia rekodi ya kutwaa Ubingwa wa EPL UNBEATEN, pia wanashikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi za ligi kuu (49) UNBEATEN- EPL
󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿.

Arsenal pia wanashikilia rekodi ya timu za England zilizocheza mechi nyingi zaidi UEFA champions league but hawajawahi kutwaa Ubingwa.

20 ◉ Golikipa, Lev Yashin anashikilia rekodi ya kuokoa penati nyingi zaidi Duniani (140).



𝙏𝙊𝙈 𝘾𝙍𝙐𝙕
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…