Hizi ndizo siri za mafanikio ya Rais John Pombe Magufuli

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Tangu aingie madarakani takribani miezi sita iliyopita Rais John Pombe Magufuli amezidi kujizolea umaarufu ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Imenichukua muda kufanya utafiti huu ili kubaini siri iliyofichika nyuma ya mafanikio ya Rais John Magufuli.

Kitu cha kwanza, Rais Magufuli alikuwa amejiandaa na kujiamini hata kabla uchaguzi haujafanyika. Hakupenda staili ya uongozi wake kufanana na waliomtangulia.Lakini pia hakutaka aonekane mgeni Ikulu jambo ambalo alihofia lingewapa mwanya viongozi waandamizi ndani ya chama na serikali, kumkabili afate maelekezo wanayoyataka wao na siyo ya kwakwe.

Na kwamba ili afanikiwe kiutendaji, alijiuliza mwenyewe swali kwamba wananchi wanataka nini kutoka kwakwe, akagundua kuwa wananchi wamechoshwa na wala rushwa na mafisadi. Hivyo walitaka Rais ajaye afumue mtandao wa wala rushwa na kuziba mianya ya kifisadi.

Kikubwa zaidi Rais Magufuli alitambua kuwa cheo ni dhamana kwamba kila mtu anastahili kuthaminiwa utu wake, na kuona kwamba nchi inatawaliwa kwa misingi ya demokrasia na nidhamu.

Rais Magufuli alitambua tangu mapema kwamba atakutana vikwazo mbele yake kutoka kwa vigogo wazoefu wa ndani nan je ya nchi wenye ushawishi mkubwa na masalahi yao binafsi.
Ili kukwepa hilo Rais Magifuli alikwepa mtego huo kwa kujipambanua kama kiongozi asiyetaka kuingilika, akakwepa mtego wa wa wahisani (mataifa makubwa) kwa kukataa kusafiri nje ya nchi.

Awali alikataa pia kukutana na wafanyabiashara wakubwana bila kificho alitamka hakuna mfanyabiashara yeyote aliyemchangia katika mapambano yake ya kuingia ikulu.

Siri nyingine kubwa ni Uzalendo. Rais Magufuli ni mzalendo wa dhati kutoka moyoni. Hili halina ubishi kwani ukimwangalia kwa sura, maneno na matendo yake yanaakisi msimamo halisi juu ya uzalendo wake kwa taifa lake.

Aligundua kuwa Mwalimu Nyerere, hakutaka utani katika masuala yaliyogusia Taifa. Mbaya yeye (Baba wa Taifa) alitumia utaratibu wa kutumbua majipu kwa watendaji kwa lakini aliishia kuwahamisha kutoka taasisi moja kwenda nyingine. Kwake Dk. Magufuli baada ya kusoma hisia za wananchi, yeye akaamua kuchukua hatua ya kutumbua majipu kwa kuwasimisha kazi wengine kuwafukuza ili hatua za kisheria zichukue mkondo wake.

Kadhalika siri nyingine iliyojificha nyuma ya mafakinikio ya Rais Magufuli ni kujiweka mikononi mwa Mwenyezi Mungu kabla ya Kushika madaraka . Dk Magufuli alimwachia Mungu atawale maisha katika yake. Alikubali kuishi ndani ya matendo ya Mungu, na aliyejua uongozi wa nchi unatokana na matakwa ya Mungu na siyo vingine .

Inaonyesha wazi kuwa Dk. Magufuli hakwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta dawa ya kushinda urais wala kuomba kula makanisani na misikitini ilia pate msaada wa viongozi wa dini kwa ushawishi wao, alikuwa anajua kama ipo ipo tu haswa ikiwa imeandikwa na muumba.

Siri nyingine ya Dk. Magufuli, hakutaka kujenga makundi tangu achukue fomu na kuirudisha. Hakupenda kuwa na makundi ili baadaye akifanikiwa, asipate tabu ya kusumbuliwa na washauri uchwara. Alitaka mwisho wa siku ajiamulie mambo yake mwenyewe kwa kufuata kanuni na sheria za nchi.

Kwa maana nyepesi hakutaka aje kuchukua muda mwingi kulumbana na wana hisa wake. Akiacha kushughulikia mambo ya wananchi wake ambao wanamtegemea kwa asilimia kubwa kabisa katika kuwavusha kuelekea nchi yenye viwanda na maendeleo makubwa kabisa katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na Kati. Hivyo sababu kubwa ya kukwepa makundi, alikusudia kuja kufanya kazi bila kuingiliwa na wenye fedha waliomwingiza.

Mwisho kabisa nimalizie kwa kusema siri kubwa ya mafanikio yake kwa ujumla yanatokana na mapenzi ya dhati kwa nchi yake. Ameonyeshawazi kuwa huko nyuma alichukia nchi kuibiwa na kufanywa shamba la bibi ambalo halina mwewnyewe.

Hili limejionyesha wazi Tangu siku ya kwanza alipoingia ikulu kwa kukataa kata kata kutawaliwa na tama ya fedha kutoka kwa wafanyavbiashara wakubwa. Dk. Magufuli anataka ndoto zake zitimie kwa kuongoza nchi na kuiachia mafanikio makubwa huku akiwa na azma ya kutaka kuifikisha nchi katika kiwango cha kati.
 
Ndg maisha mazuri bila ya unafiki inawezakana

Vijana Lumumba FC zindukeni, mnaweza kuendesha maisha yenu bila kujipendekeza, bila kusema uongo, bila kupika majungu, bila kujitoa ufaham, mbona inawezekana jamani? Zindukeni
 
Nakuunga

Nakuunga mkono
 
Back
Top Bottom