Hivi Wizara na Taasisi za Serikali zina watu wa IT?

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,936
5,040
Watu wengi wamekuwa wakilala mika kuwa wanapata shida sana kupata mawasiliana na wizara kwa asilimia zaidi ya 98% kwa kupitia namba za simu au emails walizo weka kwenye website?
Wizara na idara karibia zote ukipiga unaambiwa hiyo simu ilisha fungwa au haitumiki tena...
Emails ndio kabisaaa hazijibiwi na sijii wameweka za nini?

Kuna wizara zenye maelekezo ya kujaza online.. kama uhamiaji nk
Hivi karibuni (mwezi Nov) hapa mkoani kwangu nili down load na kupeleka copy ofisi ya uhamiaji ya mkoa - copy ya kuomba Visa..Afisa uhamiaji akanijulisha kuwa hiyo haitumiki/imepitwa na wakati?. (ujue nilipeleka mkono kwa mkono baada ya kushidwa kuwapata kwenye simu...
Ofisi ya Waziri mkuu...namba Zote na Email zote zilikuwa hazifanyi kazi kuna watu walikwama kupata maelekezo tu ya kupata kibali cha picha...ikawabidi wafunge safari ya dar (ghrama zaidi ya laki tano) wangepata tu kwa simu...sija jaribu tangu ameingia huyu mpya

SWALI LANGU NI JE? IDARA ZA SERIKALI KUNA WAFANYAKAZI WA INFORMATION TECHNOLOGY (IT??) na kama wapo wanafanya kazi gani? isije kuwa tunalipa mishahara bureee au wamepewa kazi bila kujua wajibu wao....
Kwaa taarifa tu, Mashirika ya private namba zao za simu na email walizo weka kwenye website zinafanya kazi kwa aslimia 98% na hiyo mbili pengine ni matatizo ya shirika la simu husika/kuharibika au signal
 
Kaka am talking from what i know....suala la watu wa IT ni teknolojia tu...kwamba kuhakikisha director ana email adress sasa linakuja suala la huyo alopewa hiyo email anaitumia??hapo huwezi walaumu IT's....mfano mwingine taasisi ina website hapo tayari IT washafanya kazi yao sasa suala la content ya hiyo web sio la watu wa IT tena litakua ni la afisa habari wa taasisi kuhakikisha web ipo updated na realtime information....thats how things are supposed to work broo
 
Bwana Jim
nashukuru kwa kulitolea ufafanuzi japo bado naona kwamba moja Idara zilizo jipanga zinatakiwa ziwe na utaratibu ambao IT anaweza kujua mabadiliko yanayotakiwa kufanya kwenye website.
Ukweli...kama wanapitia huku nawakumbusha kuwa website za Serikali na mashirika yake...nyingi zipo outdated...
Wazipitie na kuziupdate kila wanapopata mabadiliko...
Ili kwendana na hii kasi ya muheshimiwa Raisi ya kuwarahisishia wananchi
 
Mmmmh unasema ulienda uhamiaji kuomba VISA!!?Wewe sio raia wa tz?
Hapana, sijaenda uhamiaji kutafuta Visa yangu...Ila nilitaka kumtumia rafiki yangu wa Ughaibuni ili ajaze...kumpatia urahisi wakati wa kuja.
Mimi ni mtanzania halisi (sio wa kuunga unga) na nina sifa ya kuongea lugha kadhaa za makabila ya kwetu tz...
 
Hapana, sijaenda uhamiaji kutafuta Visa yangu...Ila nilitaka kumtumia rafiki yangu wa Ughaibuni ili ajaze...kumpatia urahisi wakati wa kuja.
Mimi ni mtanzania halisi (sio wa kuunga unga) na nina sifa ya kuongea lugha kadhaa za makabila ya kwetu tz...[/QUOTkwani huko aliko hakuna balozi?maana kama tupo ughaibuni na anataka kuja tz anaweza kwenda kwenye balozi akapata visa au akapata siku anawasili tz.
 
Kumbe information technology?nilidhani magari yale ya kwende nchi za nje kupitia bandari zetu
 
Bwana Jim
nashukuru kwa kulitolea ufafanuzi japo bado naona kwamba moja Idara zilizo jipanga zinatakiwa ziwe na utaratibu ambao IT anaweza kujua mabadiliko yanayotakiwa kufanya kwenye website.
Ukweli...kama wanapitia huku nawakumbusha kuwa website za Serikali na mashirika yake...nyingi zipo outdated...
Wazipitie na kuziupdate kila wanapopata mabadiliko...
Ili kwendana na hii kasi ya muheshimiwa Raisi ya kuwarahisishia wananchi
Kaka ni vema ungetafiti kidogo mgawanyo wa majukumu na utendaji kazi serikalini kabla ya kutoa lawama. Kama hukijui usilalame bure. Unadhani IT ndo anajua content za website zinapaswa kuwaje au ndo anaeandaa form unazojaza? Au ndie anye enforce matumizi ya tehama kwenye taasisi? You have a point ila umeipeleka sio sehemu husika.
 
Huyu atakuwa ni mmojawapo coz majibu yao ndo huwa dizain hiyo. Mteja anataka apate huduma, mambo ya utendaji na mnavyogawana majukumu inamhusu? Kazikwelikweli!!
 
Huduma anaitafuta jamii forum? Angeenda kwa wahusika wangempatia huduma unataka jamii forum ndo watu waweke hizo taarifa? Guys be serious bana. Pia hapa hakutaka huduma alilaumu watu wa IT. Think big mkubwa.
 
Watanzania ni wagumu kuelewa maandishi...narudia kazu ya watu wa IT serikalini ni technology tu na sio content ya website ama systems...anaepaswa ku update web ni P.R.O wa taasisi...na pia sio kazi ya watu wa IT kuenforce matumizi ya technology..
 
  • Thanks
Reactions: OR7

Hawawezi kuelewa maana watanzania ni wavivu wa kusoma.
 
Watu wengi wamekuwa wakilala mika kuwa wanapata shida sana kupata mawasiliana na wizara kwa asilimia zaidi ya 98% kwa kupitia namba za simu au emails walizo weka kwenye website?
Wizara na idara karibia zote ukipiga unaambiwa hiyo simu ilisha fungwa au haitumiki tena...
Emails ndio kabisaaa hazijibiwi na sijii wameweka za nini?

Kuna wizara zenye maelekezo ya kujaza online.. kama uhamiaji nk
Hivi karibuni (mwezi Nov) hapa mkoani kwangu nili down load na kupeleka copy ofisi ya uhamiaji ya mkoa - copy ya kuomba Visa..Afisa uhamiaji akanijulisha kuwa hiyo haitumiki/imepitwa na wakati?. (ujue nilipeleka mkono kwa mkono baada ya kushidwa kuwapata kwenye simu...
Ofisi ya Waziri mkuu...namba Zote na Email zote zilikuwa hazifanyi kazi kuna watu walikwama kupata maelekezo tu ya kupata kibali cha picha...ikawabidi wafunge safari ya dar (ghrama zaidi ya laki tano) wangepata tu kwa simu...sija jaribu tangu ameingia huyu mpya

SWALI LANGU NI JE? IDARA ZA SERIKALI KUNA WAFANYAKAZI WA INFORMATION TECHNOLOGY (IT??) na kama wapo wanafanya kazi gani? isije kuwa tunalipa mishahara bureee au wamepewa kazi bila kujua wajibu wao....
Kwaa taarifa tu, Mashirika ya private namba zao za simu na email walizo weka kwenye website zinafanya kazi kwa aslimia 98% na hiyo mbili pengine ni matatizo ya shirika la simu husika/kuharibika au signal

Kuna tatizo kubwa sana kwenye IT Tanzania. Inabidi JPM afanye kazi kubwa sana kubadili mfumo ili ofisi zote zitumie machine haya mambo ya kubeba makaratasi yamepitwa na wakati tubadilike tena haraka sana, hii ni project kubwa sana on its own. Haiwezekani mtu anaingia ofisini halafu hata hafahamu e-mail zimeingia ngapi kwenye inbox yake na kuzifanyia prioritisation, then kuna advantage ya kufanya kazi ukiwa nyumbani au mahali popote through your office laptop. Haya yote yanawezekana ni kuamua tu kufanya lazima tujaribu kuiga mfano kwenye nchi zilizoendelea.
 
Kwa kweli ina kera sana...
Mtoto aliye faulu anatoka Songea kutafuta fomu ya kujiunga kidato cha tano Weruweru sekondari - Kilimanjaro? au anakwenda shule bila kujua mahitaji eti anasubiria barua ya posta??? haiingii akilini kwa hii karne ya 21???

Ka website ka shule hata laki mbili inatosha kukaweka hewani?
Maelezo mengi ya shule ni copy paste...hakuna ubunifu hapo...ni information tu zinatakiwa
Tubadilikeni jamani...
 
Back
Top Bottom