Kuwa na rafiki wa kweli mwenye 98% ni muhimu sana katika maisha yako. Njia ya kumjua rafiki wa kweli hutokana na mapito katika maisha yako wewe binafsi. Rafiki wa kweli utamtambua kuanzia mwaka mmoja mpaka miaka mitano.
Je una rafiki/marafiki? Je wewe ni rafiki?
Sifa na tabia za rafiki wa kweli.
Hufurahia mafanikio ya rafiki yake
Anamkubali rafiki yake jinsi alivyo
Sio omba omba (fedha/vitu)
Anaelewa urafiki ni barabara mbili ya kwenda na kurudi
Sio mbinafsi
Yuko tayari kumsadia rafiki yake 100%
Hamwongozi rafiki yake kutenda mabaya
Hamkimbii rafiki yake anapopata matatizo/shida
Hamkimbii rafiki yake anapokuwa katika raha
Hamtafuti rafiki yake pale tu anapokuwa katika matatizo au shida
Anaye omba msamaha kwa rafiki yake kama amekosea
Hamnenei rafiki yake maneno ya uongo
Hamtendei rafiki yake mambo asiyopenda kutendewa
Je una rafiki mwenye sifa na tabia hizo? Wewe je una tabia sifa hizo?
Ili uweze kuwa na marafiki wa kudumu na kuenjoy uwepo wao katika maisha yako ni lazima wawe/uwe na tabia, sifa hizo 13.
Sihitaji marafiki nahitaji business partner sababu marafiki wa kawaida kukukimbia wakati wa shida ni kawaida na inaumiza sana ikitokea bora business partner akikimbia utajua kuwa mambo yalikuwa hayamlipi so hana budi kuenda mbele na mi nitamuelewa.
...wengi inatubidi "kuchekeana kinafiki" tu,wakati unajua kabisa jana alikusemea uongo kwa wengine,ila unapotezea tu.Ukijidai unatafuta rafiki mwenye hizo sifa hapo juu,utasubiri milele.!!
Ninae mmoja tu wa aina hiyo.......sikufanikiwa kupata zaidi......nilikuwa na 2 mmoja akanisaliti......sasa kabaki Mamushka pekee yake......Luv you my super best friend.......
Huyu ni rafiki yangu wa kweli. Ananiita rafiki, mpenzi, ndugu na kila kitu. Hata kama sina pesa hali ya mahusiano haibadiliki. Ni mvumilivu kweli kweli.
Asante sana kwa kuwa rafiki na mpenzi wa kweli lakini sitakutaja hapa.
When it comes to loyal friends: God has given me more than what I deserve. He has favored and blessed me with true friends whom I can proudly call "sisters". I'm too grateful for my girls