Hivi wewe ni rafiki wa kweli 98%

Jajojo

Senior Member
Sep 1, 2015
155
95
Kuwa na rafiki wa kweli mwenye 98% ni muhimu sana katika maisha yako. Njia ya kumjua rafiki wa kweli hutokana na mapito katika maisha yako wewe binafsi. Rafiki wa kweli utamtambua kuanzia mwaka mmoja mpaka miaka mitano.

Je una rafiki/marafiki? Je wewe ni rafiki?

Sifa na tabia za rafiki wa kweli.

  1. Hufurahia mafanikio ya rafiki yake

  2. Anamkubali rafiki yake jinsi alivyo

  3. Sio omba omba (fedha/vitu)

  4. Anaelewa urafiki ni barabara mbili ya kwenda na kurudi

  5. Sio mbinafsi

  6. Yuko tayari kumsadia rafiki yake 100%

  7. Hamwongozi rafiki yake kutenda mabaya

  8. Hamkimbii rafiki yake anapopata matatizo/shida

  9. Hamkimbii rafiki yake anapokuwa katika raha

  10. Hamtafuti rafiki yake pale tu anapokuwa katika matatizo au shida

  11. Anaye omba msamaha kwa rafiki yake kama amekosea

  12. Hamnenei rafiki yake maneno ya uongo

  13. Hamtendei rafiki yake mambo asiyopenda kutendewa
Je una rafiki mwenye sifa na tabia hizo? Wewe je una tabia sifa hizo?

Ili uweze kuwa na marafiki wa kudumu na kuenjoy uwepo wao katika maisha yako ni lazima wawe/uwe na tabia, sifa hizo 13.

“marafiki wanakukimbia au wanakukimbilia”


ianyelwisye@gmail.com
 
Sihitaji marafiki nahitaji business partner sababu marafiki wa kawaida kukukimbia wakati wa shida ni kawaida na inaumiza sana ikitokea bora business partner akikimbia utajua kuwa mambo yalikuwa hayamlipi so hana budi kuenda mbele na mi nitamuelewa.
 
...wengi inatubidi "kuchekeana kinafiki" tu,wakati unajua kabisa jana alikusemea uongo kwa wengine,ila unapotezea tu.Ukijidai unatafuta rafiki mwenye hizo sifa hapo juu,utasubiri milele.!!
 
Ninae mmoja tu wa aina hiyo.......sikufanikiwa kupata zaidi......nilikuwa na 2 mmoja akanisaliti......sasa kabaki Mamushka pekee yake......Luv you my super best friend.......
 
Duniani sina rafiki wala ninae mwamini sana..... kosa hela ndio utajua rafiki wa kweli ila ni .0005%
 
Huyu ni rafiki yangu wa kweli. Ananiita rafiki, mpenzi, ndugu na kila kitu. Hata kama sina pesa hali ya mahusiano haibadiliki. Ni mvumilivu kweli kweli.
Asante sana kwa kuwa rafiki na mpenzi wa kweli lakini sitakutaja hapa.
 
Rafiki wa kweli ni LANGA

Matawi ya juu pumzika kwa amani LANGA!
 
When it comes to loyal friends: God has given me more than what I deserve. He has favored and blessed me with true friends whom I can proudly call "sisters". I'm too grateful for my girls
 
Back
Top Bottom