Hivi Wanaume Mnaangaliaga Nini?

Mom Fay

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2014
Posts
1,059
Reaction score
316
Habari humu ndani.

Wanaume nisaidieni jamani na wadada pia, maana nakuwa kama sielewi elewi. Hivi mnapoamua kuoa au kuingia kwenye mahusiano na mwanamke mnaemchagua mwenyewe mpaka ndoa huwa mnaangalia nini?

Nauliza hivi kutokana na kinachoendelea hapa mtaani kwetu, kuna wadada wa tatu, wawili kiumri wanaenda miaka 30 sasa, na mmoja ana 26, hao wawili ni warembo balaa, wazuri, wana shepu za hatari, hadi wanaitwa visu, kitabia nawaona kawaida tu.

lLkini hadi leo hakuna hata dalili za mnuso wala ndoa wapowapo tu wenyewe wanadai mda wao bado,huyo mwenzao sasa, chembambaa, pasi si pasi akisimama mbele kama nyuma, viziwa kama havipo vile, sura ngumu lakini navyoandika hapa tupo jikoni tunarekebisha mambo ya tumbo anachukuliwa na rubani.
 
na mimi nasubili jibu la hili swali..wanaume njoo mfunguke ili tujue jamani.
 
mke mwenzangu tema mate chini/mwenzio akinyolewa we tia maji/mwenzio akilia we tulia...huyu mume wetu hatujui kama atatuoa au vipi....mi sitii neno hapo

Salama lakin?
 
Labda wanapenda wasipopendwa maana ndoa ni connection inakuja kwa maelewano na upendo mlionao.
 
Kwanza, hao visu wanahitaji ndoa?

Na kama wanajitaji, wanahitaji wenza wa aina gani? Na aina ya watu wanaowahitaji wapo kwenye mzunguko wao wa maisha?

Na kama wapo, hao wenza wanahitaji aina ya wadada kama hao visu?

Kimahusiano ya kimapenzi, binadamu tuko tofauti. sana.
 
kila ndege anatua kwenye mti aupendao
 
wengi wa wanawake wazuri wanapenda starehe na makundi yasiyo na mpango hivyo hata unapotaka kukutana nae kwa mara ya kwanza hukimbilia sehemu za gharama hili sio tatizo sana ila shida ni pale kila weekend anataka kubadilisha viwanja vya kuzurura na kutumia pesa unakuta mwanamke anajua saluni nyingi bar nyingi hotel nyingi club nyingi kuliko plot zinazouzwa ili mjenge ndio maana tunakimbilia hao unaowaona hawana mvuto.
Unakuta mwanamke anapiga picha makalio anapost kwenye social network huyo nae aolewe umesikia nyumbani kwangu napiga baikoko au nafungua bendi ya muziki. Tabia za wanawake wanaojiona wazuri ni za hovyo
 
mh hawaangaliag shepu uzuri wala ubaya... bt atlist u smart wa ke na kingne hisia juu ya huyo dem..I.e upendo
 
mke mwenzangu tema mate chini/mwenzio akinyolewa we tia maji/mwenzio akilia we tulia...huyu mume wetu hatujui kama atatuoa au vipi....mi sitii neno hapo

Salama lakin?

kweli mke mwenza,.. salama tu!!.
 

thanks much!
 
Unapost makalio yako mtandaoni then unategemea ndoa.Bitch utakuja utongozwe ukawe stripper club.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…