Kitendo alichofanya mwekezaji huyo ni cha kinyama sana! Amenisikitisha sana kwani baada ya ukatili alioufanya anaeleza kuwa ana 'lease' ya eneo lile na analilipia! Kwanini asitoe taarifa kwa uongozi wa eneo hilo ili wananchi wachukue tahadhari hasa ukizingatia kuwa eneo lile halikulimwa muda mrefu. Poleni watanzania wenzangu kwa hasara kubwa mliyopata. Pole yetu pia watanzania kwa maliasili yetu iliyoangamizwa kwa ubinafsi na jeuri ya mwekezaji. Ninawaombea wale watoto wote waliolazwa kwa athari ya sumu ili MOLA awaponye.
.