Hivi unaweza ukajua Kingereza vizuri na ukawa huna pesa hata za mboga?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,583
44,827
Wengi tumesoma secondary na vyuoni na wengine mpaka international school wamepita lakini kiukweli hatujui kuongea english ipasavyo wengi tunakielewa kwa kukisoma pekee na sio kuongea.

Mimi nimekaa nimefikiria nimeona sijawahi kuona mtu anajua kingereza kukiongea halafu awe maskini hio haipo. watu wakijua unakiweza kingereza utapatiwa fursa nyingi sana maboss wengi watatamani kukaa na wewe wajifunze mengi maana ni lugha inayovutia sana hata ukikaa bar kingereza kinanoga sana achilia mbali ukalimani na kuongoza watalii wa kizungu hela ipo nje nje.

Mimi nimeona kila deal nalowaza naona kama halilipi ma bitcon ma free lancing yote naona nimeshapishana nayo kushoto ngumu kujifunza zinahitaji muda ila kingereza rahisi kujifunza kwani ni kukiongea tu achana na waswahili watakuona una dharau siku hizi kiswahili hukipendi ila we wapotezee hakikisha watu unaokutana nao wako interest kujifunza piga nao story soma machapisho mengi angalia movies zenye subtitle baada ya mwaka we utakuwa level nyingine na uhakika kitakupa hela.
 
Kuanzia kule kule chuo kuna watu wanapiga ngeli halafu wanamwaga ung'eng'e halafu kichwani empty head.
Hao ndio sasa wakishamaliza chuo huwa wanamwaga lugha ya malkia kwenye mabanda ya gongo na mabar.
 
Kwani kiingereza ni pesa?

Watumishi kibao wanajitutumua kusomesha watoto english medium kuanzia low level mpaka high school lakn hiwapi utajiri,

Utajiri au ukwasi huja na mapambano ya mtu yawe halali au haramu, ila sio kujua lugha.

Unaweza kujua english vizuri maana ile ni language mazigira ndio yanakufunza language na unaweza kujifunza language yoyote kulingana na mazingira umekuwa exposed, hata wabongo wanaoenda kwa madiba wakikaa miaka 3 wanajua kizulu, wakikaa miaka 10 wanaongea kizulu vizuri tu kwasabab mazingira yanakulazimu.

Hitimisho
Lugha haina influence yoyote kwenye mafanikio yako., bali ni uwezo wa akili yako kutumia na kuona fursa zilizopo kwenye jamii yako ndio zitakutoa kimaisha.

Gademn
 
Hao wanajua juu juu mkuu mimi nasemea wale wanaongea fluently yaani hasitisiti anayezingatia grammar na tenses kwa 100%
Unachotakiwa kujua watu wenye pesa ni wafanyabiashara asilimia 90, na hawajasoma hawajui hivyo vingereza vyenu.
 
Back
Top Bottom