Baada ya dalili za rasharasha za kuvunjika kwa Ukawa wakati wa uchaguzi wa Oct 2015 kwa baadhi ya majimbo kusimamisha mgombea zaidi ya mmoja kama Masasi Mtwara na Ukonga Dar hali iliyosababisha kuyapoteza majimbo hayo sasa hali ya kusimamisha mgombea zaidi ya mmoja kwenye uchaguzi wa madiwani ambao kampeni zake zimeanza hivi karibuni imejitokeza kwa nguvu sana. Je hali hii haimalizii misumari ya mwisho kwenye jeneza la Ukawa hivyo kuipa CCM uwanja mpana zaidi ws kuongoza nchi kwa muda mrefu na kuufuta kabisa upinzani legelege nchini na kufungua njia kwa upinzani komavu utakaoleta maendeleo ya kijamii na uchumi tuliyoyatarajia?
Je hii sio nafasi nzuri kwa vijana wasomi wenye vuguvugu la upinzani wa kweli kuwaondoa viongozi wa sasa wa upinzani kwa nguvu ya hoja ya kushindwa kuunganisha upinzani kama walivyoahidi?
Je hii sio nafasi nzuri kwa vijana wasomi wenye vuguvugu la upinzani wa kweli kuwaondoa viongozi wa sasa wa upinzani kwa nguvu ya hoja ya kushindwa kuunganisha upinzani kama walivyoahidi?