Hivi ufalme wa BB(Blackberry) umeishia wapi??

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
17,049
21,526
Salam wakuu,
Habari za wakati huu? Strait to the point, miaka ya nyuma kidogo simu Aina ya blackberry zilishika hatamu Sana. Wakati tuko vyuoni sifa ya pisi Kali au blazamen lazima umiliki BB.

Pamoja na kwamba ilikua inakera hususani kwenye swala la kureboot unaweza ukalia mpaka simu iwake, lakini kilichowakamata wengi Ni BBM. Aisee, ile ilikua ndio swaga wakati huo. Manzi humuombi namba Bali BBM pin, mpaka kukawaga na ma BBM party etc.

Sasa nashangaa sahivi sizioni kabisa, nimejaribu kuingia play store naona hata BBM kutumia inabidi ulipie. Sasa sijui wakuu Kuna Nini kuhusu hii kampuni
 
Kila zama na wakati wake mkuu! Wako wapi kina ZTE na HTC? Washkaji walikua na mashine hatari sana kwa kipindi hicho lakini nao zama zao zishapita, lakini kuna kampuni nyingi tu za simu za kisasa wanatengeneza simu zenye features za hovyo au kulingana na hiyo miamba ya wakati huo, Nokia, LG & Sony Xperia kidogo wanaenda na nyakati kimtindo..
 
Sahihi mkuu, enzi hizo htc one daah
 
Kweli mkuu naona department zao za R & D zinafeli Sana. Wajaribu hata kuclone wenzao, kisoko inaruhusiwa. Hata Oppo zamani UI ilikua Ni iOs tupu yaani.
 
For reals Holmes, ile GUi ya kishenzi plus karibu kureboot simu uone. Unaweza ukaenda tutorial, ukarudi, unafanya assignment ukamaliza, ukaenda presentation jioni ukarudi, bado haijawaka.
 
Unaendelea kujengeka katika magari yanayojiendesha (autonomous vehicles). Blackberry wanamiliki software inaitwa QNX ambayo ipo katika magari zaidi ya milioni 175. Kadri jambo la kujiendesha magari linavyozidi kusambaa ndio thamani yake inapanda zaidi kwa kuwa hadi sasa hamna software secure ya magari kama yao.
 
Kwanza huo mfumo tu wa mabatani mengi kama keyboard ya computer nilikiwa nachukia kinyama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…