Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,389
- 38,667
CCM ni chama kwa ivo unapoitaja CM unaashiria kuitaja taasisi kwa kufuata mfumo wake wa kiungozi (hierarchy) na maamuzi yanayofanywa na walio viongozi. Maamuzi ya CCM hutokea kwenye vikao kwa kufuata demokrasia ya chama hicho. Kwa mantiki hiyo siyo kila mwana CCM ni CCM ingawa wana CCM ndiyo wanaiunda CCM.
Upande mwingine wapo wana CCM ambao ndiyo wanaiunda CCM. Kwenye kundi hili wapo wale walio kwenye uongozi na wale wasio viongozi. Tunaposema kwamba tunaongozwa na CCM tunaamini kwamba CCM ndiyo iliwaleta wana CCCM ambao waligombea nafasi mbali mbali wakati wa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Swali la msingi ni kwamba hawa wana CCM wanaoongoza nchi hivi sasa wanadhibitiwa na chama chao? Kwa mfano Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dar es salaam imeshakaa na kutafakari tuhumu anazopewa Mkuu wa Mkoa huo kwamba ameghushi vyeti vyake vya elimu? Jee kama CCM Dar haijakaa tunawezaje kuendelea kuamini kwamba CCM ndiyo inaongoza nchi na wala si wana CCM walioletwa na chama hicho?
Au kwa kujua kwamba zama hizi CCM haiwadhibiti wanachama wake na kuwasimamia kuongoza nchi ndiyo maana kwenye uchaguzi wa Mwaka 2015 John Pombe Magufuli alijitenga na kujinasibisha na jina la chama hicho. Jee 2020 CCM inaweza kuomba kura kama chama ama wana CCM wataomba kura kama watu binafsi?