Hivi TBL mnafikiria nini kupunguza ujazo wa Castle Lite kutoka 375ml hadi 330ml?

Baba Heri

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
1,098
2,000
Baada bia ya Serengeti Lite kupendwa na wateja wengi licha ya kuwa na ujazo mdogo (330ml) naona sasa TBL wameona nao wapunguze ujazo wa Castle Lite kutoka 375ml hadi 330ml.

Aisee kama mnadhani bia hupendwa kutokana na ujazo mdogo hapo mtakuwa mmechemka nawashauri hata huyo aliyetoa hilo wazo mchunguzeni pengine anatumika.
 

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
954
1,000
Mi napenda Sana castle light shida ilikuwa ujazo, kwakuwa Sasa wamepunguza, mtanikuta nimelalaa mtaroni.
 

GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
2,442
2,000
Kuna vitu viwili hapo wamefanya kwa pamoja. Na ni kawaida katika biashara kumfwata mpinzani wako kwa kupunguza bei/ujazo au kupunguza bei & ujazo vyote kwa pamoja.

Labda ungetuelezea Castle lite 375ml ilikua Sh ngapi na Serwngeti Lite 330ml ilikua sh ngapi na sasa Castle Lite 330ml ni Sh ngapi.

Pengine wameona kushusha bei ili waendane na Serengeti yenye 330ml haiwezekani kwahiyo inawabidi wapunguze na ujazo pia
 

Wise E

JF-Expert Member
May 10, 2019
693
1,000
Baada bia ya Serengeti Lite kupendwa na wateja wengi licha ya kuwa na ujazo mdogo (330ml) naona sasa TBL wameona nao wapunguze ujazo wa Castle Lite kutoka 375ml hadi 330ml.

Aisee kama mnadhani bia hupendwa kutokana na ujazo mdogo hapo mtakuwa mmechemka nawashauri hata huyo aliyetoa hilo wazo mchunguzeni pengine anatumika.
castle lite ladha yake inanizinguaga kitu serengeti lite mzigo kwenye kindoo wabaridi naogelea tuu mzigo wa elfu kumi weekend inakuwa muluwa kabisa
 

Sir Khan

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
5,133
2,000
Kisa bia tu lakini unavyolalamika sasa utafikiri umenyimwa mafao yako Nssf.
Joking.
 

Genisys

Senior Member
Oct 14, 2015
156
225
Mbinu za kibiashara tu hizo mkuu, Serengeti Lite 330ml anauza sana. Yaweza ikawa sababu ya Castle Lite kupunguza ujazo aweze kucompete vzr


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
11,813
2,000
Lengo ni kuweza kushindana bei na mpinzani; mpinzani wako ana ujazo mdogo huwezi kushindan naye kwa bei wakati wewe una ujazo mkubwa; itakubidi uuze ghali zaidi. Kwa kuzingatia hulka ya watanzania kutokuwa wadadisi; kwamba wao wanachoona ni bei bila kuchunguza kujua specs za hiyo product like volume hivyo ku-justify price hakuna namna nyingine zaidi ya kuwapunguzia specs ziwe sawa na za mshindani wako maana wanachojali ni unafuu wa bei na sio zaidi. No wonder nchi hii inaongoza kwa bidhaa fake!
 
Top Bottom