Hivi Tanzania bado tunajisifu kwamba tuna demokrasia?

mtima nyongo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
1,947
2,047
CCM, tunajua ya kuwa imeshindwa Zanzibar. Je, kwa nini wanang'ang'ania madaraka huku tukijisifu kuwa tuna demokrasia?
 
CCM tunajua ya kuwa imeshindwa Zanzibar. Je, kwa nini wanang'ang'ania madaraka huku tukijisifu kuwa tuna demokrasia?

Demokrasia ipo, lakini ni pale tu CCM walishindwa Z'bar na bara. Na mnaruhusiwa kugombea nafasi zote kasoro Urais, Umeya na Ubunge. Ni shida tu zinawafanya wakubali. Mmemsikia Samia Suluhu alisema wakati bwa kampeni kwamba wapinzani hawatapata kitu kwenye utawala wao.
 
CCM tunajua ya kuwa imeshindwa Zanzibar. Je, kwa nini wanang'ang'ania madaraka huku tukijisifu kuwa tuna demokrasia?

Unaongelea demokrasia ipi, ya marafiki zenu wazungu? Ama demokrasia inayopambana na wadhalimu wananaotumiwa na wazungu kuharibu usawa wa kiafrika!

Tena, tuna demokrasia kubwa sana na ya kuigwa.
 
demokrasia ipi unayomaanisha?...

aristocratic rule, democratic rule au authoritarian rule?...kumbuka zote hizo zinatumika kuongoza watu na kila moja inayo faida na hasara yake dogo...
 
Yaani watu wazima na akili zao bado wanajadili kwa sababu gani Jambazi Sugu hakushinda? Au kwa nini Zanzibar wanarudia uchaguzi. Hivi wanafikiri nchi zinaota kama uyoga? Grow up! Hizo peremende mnazopewa zina mwisho. Hata huko mnakosifia demokrasi mnasikia tu mmejionea mambo yanavyokwenda? Wacheni unafiki mmekalia majungu badala ya kuandika mambo yatakayosaidia hii nchi kuendelea. Uchaguzi wa rais wa Tanzania umekwisha sasa ni Kazi TU.
 
Hakuna demakrasia huku dolacrasia .domocrasia tanzania haijawahi kuwepo mbona tumevya uchaguzi inateuliwa navraisivaliyeko madarakani .haha haa sikubtanzaniavikija demokrasia na kiama ndio itakua tayari
 
Demokrasia ipo sana tu ila wewe umeangalia kwa upande wa zenj

Tena kwa mahaba yako ya yule unae mtaka

Ndio maana kuna vikao vya majadiliano
 
CCM, tunajua ya kuwa imeshindwa Zanzibar. Je, kwa nini wanang'ang'ania madaraka huku tukijisifu kuwa tuna demokrasia?
Jibu ni jepesi tu, tafsiri ya neno demokrasia kwa CCM, hususani kwa nafasi ya Urais, ni lazima wao ndiyo watangazwe washindi.

Rejea kauli zifuatazo zilizowahi kutolewa na makada maarufu ndani ya CCM.

Zanzibar kamwe haitakuja kutolewa kwa vijikaratasi vya kupigia kura.
By mwanamama Asha Bakari kwenye Bunge Maalum la Katiba mwaka 2014 kule Dodoma.

CCM tunaweza kuruhusu wapinzani wapate baadhi ya Madiwani na wabunge, lakini kamwe hatuwezi kuthubutu kumruhusu Mpinzani kwenda Ikulu.
By Bulembo, kwenye kampeni za Urais, kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

CCM iwe isivyo ni lazima ishinde uchaguzi mkuu, hata kama itafunga goli la mkono.
By Nape, kwenye kampeni za Urais kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Haya matamshi tumeyahifadhi, ili pale yatakapohitajika kama ushahidi kule The Hague Uholanzi, dhidi ya wale waliyoyatamka, tuweze kuyawasilisha kwa Bensouda.
 
Kifupi ni kwamba, Afrika hatujawahi kukubali demokrasia.

Ni kwasababu ya shida ya kuombaomba Ulaya ndio maana tunajidai tuna demokrasia.
 
Ukifahamu maana ya neno demokrasi ndio uje hapa kuanza kuhubiri. Hizi propaganda watu wanalishwa tu kila uchwao basi wanarukaruka na kusema mahali fulani kuna demokrasi nk. Ukijua maana ya hilo neno then anza kuangalia hao wanaojiita wana demokrasi uwaulize kwa nini hadi leo hii wanakubali kununua bidhaa kutoka nchi masikini kwa bei ambazo sio sahihi? Leo hii technologia yote ya simu za mkononi inategemea madini kutoka Congo, jiuliza kwa nini Congo hadi leo hawako imara na ni masikini? Europe na USA hawawezi kutufundisha sisi demokrasia wao ndio waje kwetu wajifunze. Kama nilivyosema hapo awali Tanzania haikuota kama uyoga.
 
hakuna demokrasia TZ, hata kwenye hvyo vyama vyako vinavyojiita vya demokrasia, wanakataa miswada bungen kuptishwa kwa 'kura ya saut' ila wao wanakuja kumptisha mgombea wa urais kwa kura hyo hyo, tena wanamalizia kwa kusema 'HAKUNA MJADALA', kifupi ni kuwa vyama vyote vya siasa TZ, havina demokrasia, ni unafiki 2, wote wana2mia "nkurunzinza formula"
 
Pia lowassa alisema msiwe na wasiwasi, ninyi kazi yenu kupiga kura tu. Asubuhi tu nachukuwa urais huku akijua amekwapua demo ndani ya chama chetu pendwa. Kilichokuwa kinapambana na ufisadi na mafisadi.

Pia, kuna ishu ya kumuweka agombee urais bila kupingwa kama kagame na sasa amesema yeye ndo anasimama tena 2020.

Kweli taifa halina demokrasia.

Back
Top Bottom