Hivi siku hizi kuna mwanaume anamtongoza mdada kwa kuanza na kibwagizo cha Samahani dada?

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,702
36,127
Nimekumbuka ilikuwa mwaka 2002 au 2003 nilipoitiwa mtoto (demu) aliyetoka Dar. Uncle wake ndiye aliyeniunganishia. Aise! Niliishia kutetemeka kama nimeshikwa na ngiri. Wakati huo nilikuwa Primary na sijamjua mwanamke bado. Kama yule binti angeendelea kukaa pale aliponikuta hakika ningezimia kwa hofu.

Turudi kwenye swali, hivi siku hizi ile staili ya kutongoza kwa kuanza na kibwagizo cha Smahani dada bado inatumika?
 
Hakuna formula ya kutongoza ujue vyovyote anavyokuja hesabu zikitiki unaanza hivyo hivyo hata kama ni kwa kupiga chafya
 
Kuna rafiki zangu wakenya huwa wananiambia sisi watanzania huwa tunatanguliza neno "samahani" na " naomba" kwenye kila jambo.

Hata kama mtu atakwenda dukani anataka kununua kitu atasema, naomba unisaidie kitu fulani.

Eti wanasema hadi askali anapotaka kumkamata mtu anaseama " samahani naomba nikukamate

Watanzania wakarimu sana.
 
Ilo neno LA kawaida si wengine tukikaa maskani utaskia



Psiiii !!! Psiiii oyaaa sister naomba simama kidogo halafu hapo unajifanya umemfananisha ila mazungumzo yaanzie mbali kidogo



Halafu mengine yanaendelea
 
Back
Top Bottom