Hivi shule kuwa na wanafunzi 800+ huku walimu ni wanne tu ni halali kweli.

mwalukuni mchanyato

JF-Expert Member
May 15, 2013
404
230
Habari.Tumeshuhudia nchini baadhi ya shule za msingi zikiwa na wanafunzi wengi ila idadi ya walimu ni ndogo.Mfano unakuta shule ina wanafunzi 800 na zaidi huku walimu wanne au watatu.
Hivi kwa ikama hii ya walimu,Je tunaweza kufikia malengo ya kuwapa watoto wetu Elimu bora?Ukichukua idadi hii ya walimu ni kweli wanaweza kubeba Mzigo huo wa idadi ya wanafunzi wengi hivyo?
Serikali yetu sikivu hebu tupieni jicho huku kwenye msingi wa Elimu na kama inawezekana shusheni baadhi ya wale waliojirundika kule sekondari waende kusaidia kule chini au toeni ajira zaidi kuondoa tatizo hili.
 
Kipaumbele ni madawa ya kulevya na watumishi hewa kwanza, hao acha wasote kidogo hadi 2020 watafikiriwa labda.
 
Back
Top Bottom