Kinjekitile junior
JF-Expert Member
- Apr 20, 2015
- 4,404
- 581
Ndugu wanajamvi nikiwa mfuatiliaji wa mambo ya Siasa zetu za Tanzania huwa nashangazwa sana na kitendo/vitendo vya wanasiasa kutoa lugha za kuudhi hasa wakati wa Mikutano ya Siasa na Kampeni. Wengine hufikia hatua ya kutoa matusi ya nguoni kwa washindani wao na Pindi wanapochukuliwa hatua na Mamlaka zinazohusika wanalalamika eti wanaonewa.
Najiuliza sana hivi ukiwa Mwanasiasa ndio unakuwa na kibali cha kutukana wenzio hadharani?
Mi nachojua Maadili ya Uchaguzi ya Mwaka 2015 yaliyosainiwa na vyama vya Siasa 22 kupitia Tamko la Vyama vya Siasa Tarehe 27/07/2015, pamoja na mambo mengine linapinga vikali; Matumizi ya lugha za Matusi, Uchochezi na zenye kuhamasisha Vurugu, lugha za Kashfa na Kejeli na YANASISITIZA ZAIDI VYAMA KUNADI SERA WAKATI WA KAMPENI NA SI VINGINEVYO.