Hivi nani Aligundua kutukana(Mitusi)!

No Escape

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
6,663
7,774
Yaani hili swali huwa najiuliza sipati jibu,Hakuna shule yeyote wala chuo chotechote nimewahi kusikia duniani kinatoa cheti au Degree ya mitusi. Nastaajabu sana binaadamu tuna misamiati mingi ya mitusi na tena tunajua mpaka tafsida zake hakuna binaadamu asiyejua kutukana siku hizi mpaka watoto wadogo wanatisha usiwaingie kichwakichwa kwenye hii fani>Naomba leo wana J.f mnifungue macho labda kuna watu wanagundua mitusi mipya kila mwaka wanaileta huku Duniani!
 
Hata Hili pia ni tusi

17952776_886865604788665_6314962002194466110_n.jpg
 
Matusi ukiachunguza kwa ndani hutaona sababu ya kwa nini mtu akasirike au achukie.
Mfano mtu anakuita kiungo cha uzazi cha mwanamke, sasa wewe ukasirikie nini wakati sio wala huwezi kuwa hivyo kibailojia?
Au anakuita msenge(mwanaume anaeingiliwa kinyume na maumbile) wakati wewe hauko hivyo wala haujawahi kuwa na mpango kelele na ngumi za nini hapo?

natafakari kwa nini Tusi likutoe kwenye mstari.Kurudi kwenye mada, Huu ni ubunifu wa mwanadamu ili amuudhi,amdhalilishe mwanadamu mwenzake ila kuudhika au kukasirika ni uchaguzi
 
Hakuna kitu kinachoitwa tusi duniani, Ila anayeambiwa ndio huwa anatafsri kama ni matusi au la!

Maneno ni maneno tu hakuna maneno yaitwayo matusi.

Sisi ndio tunayoyapa tafsiri.
Sio kweli, kuna sifa mtu anasifiwa na kuna matusi pia mtu anatukanwa.
 
Bado sijawaelewa kabisa,mnasema hakuna matusi! Mbona hapa jukwaani hamuandiki viungo vingine kwa jina lake?
 
Kwa mtazamo wangu mimi...

Matusi ni ile hali ya kutamka mambo ya faragha au yaliyofichwa kwa maana ya kimaadili... Hakuna tusi dogo wala tusi kubwa... Tusi ni tusi...

Tusi linaweza kutolewa kwa maana ya kusifia kitu (Excited) au kuchukizwa na kitu...

Mtu akichukia hutoa matusi kwa maana ya kuonesha amekerwa... Mtu akifurahishwa anaweza akatoa tusi kwa maana ya mihemuko (Furaha iliyopitiliza)...

Cc: mahondaw
 
Lusinde....a.k.a 'Kibajaji" Mbunge wa Mtera....mbona ni mmoja wa wahitimu Chuo cha matusi?
 
''Am tired of misionary, I dont wanna see your face''
Hapo kuna ukitafsiri unaweza kutafsiri tusi, alafu unaweza ukatafsiri kawaida. Am out
 
Hakuna matusi. It is only our reaction which matters. Ukiniambia Mimi in mjinga, sioni tatizo na tunaweza kucheka. Ila the way I will react determines Kama in tusi au la!
 
Yaani hili swali huwa najiuliza sipati jibu,Hakuna shule yeyote wala chuo chotechote nimewahi kusikia duniani kinatoa cheti au Degree ya mitusi. Nastaajabu sana binaadamu tuna misamiati mingi ya mitusi na tena tunajua mpaka tafsida zake hakuna binaadamu asiyejua kutukana siku hizi mpaka watoto wadogo wanatisha usiwaingie kichwakichwa kwenye hii fani>Naomba leo wana J.f mnifungue macho labda kuna watu wanagundua mitusi mipya kila mwaka wanaileta huku Duniani!
CHUO KIPO UFIPA. Wahitimu wa mwanzo walikuwa MDEE, LEMA, MAWAZO, KUBENEA na NASSARI. Sehemu yao ya field ni JF
 
Back
Top Bottom