Hivi mnazijua sera za CHADEMA?

Hivi mnazijua sera za CHADEMA?

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
6,909
Reaction score
4,057
10624943_1489951161260947_7576390670135654295_n.jpg

Mimi naona mission na vision za chadema hazieleweki. Leo wanakuwa na msimamo huu kesho wanabadilika. suala la kuendesha nchi linafaa kuwa na sera zinazoeleweka. Chadema sasa inakuwa na sera za matukio.

Mfano tutapiga vita ufisadi kisha hela za ufisadi zitaendeleza wananchi bila kujua wizi wa kisomi ni ngumu sana kuthibitisha mahakamani
kufanya maandamano yasio na tija. Kukataa kuunganika na vyma vingine tena kwa kashfa lakini ghafula tunawaona jangwani wakikenua meno.

Chama cha siasa lazima kiaminike na kiwe na mission na vision ila kwa chadema wamekua na sera za matukio hivo kukosa political credibility kuwakabidhi nchi yetu yenye amani na utulivu.
 
Acha kufanya maisha kuwa magumu wewe, utakuwa frustrated bila sababu za msingi.

Maisha ni marahisi sana. Mtu akikwiba ni kumpleka jela na kuzuia mali zake, mambo ya kuthibitisha yataendelea kuthibitishwa na vyombo vinavyotaka kufanya hivyo.

hieleweke, kuanzia mwaka 2015 nchi itaongozwa namna hiyo, kama kuna mtu ataonewa hiyo itakuwa ni ajari kazini, lakini hakuta kuwa na fursa ya watu kuiba alafu wanaendelea kuzungusha kende zao mitaani.

maswala ya vision na mission kama bado yanakuvutia, kasomee masters kama unayo kasome phd kama unayo kanunue vitabu ujisomee nyumbani.

umenielewa.
 
Ama kwel wkend imeanza.

Vision na mission za maccm ni zip?
Fanya comparison btn CDM NA ccm
 
Chama cha press release na matukio halafu kinataka kikabidhiwe nchi wonderful wajameni!!!!!
Haki ya nani tena , Hela ya ccm inaliwa kijinga sana ! Hivi na wewe unalipwa kwa maandiko dhaifu kama haya ?
 
Hivi mleta mada unaongelea Mission, Vission au Sera? Au unataka kujua tofauti kati ya mission, vission na sera? Nakushauri urudi darasani!
 
ukiwa na uelewa mdg ni shida

  1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika “Nguvu na Mamlaka ya Umma” (The People’s Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
  2. Aidha falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
  3. Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
  4. Historia inaonyesha kuwa “UMMA” wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
  5. CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka “Nguvu ya Umma”. Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
  6. CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa “kuchaguliwa” kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza “waliowachagua” kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
  7. Hivyo basi, falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
  8. Falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.
 
We ndio ------ wazi kweli. Ati mwenyewe umekaa ukafikiria weeee kisha ukaona umepata cha kuandika?
 
3.B. Itikadi ya CHADEMA
3.1.1 CHADEMA ni [COLOR=#009900 !important]chama
cha itikadi ya MRENGO WA [COLOR=#009900 !important]KATI[/COLOR] (center party).
3.1.2 CHADEMA ni chama kinachoamini kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi kwa kutumia raslimali za nchi yetu bila kuathiri uhuru wa Taifa, na kuhakikisha kuwa umma kwa ujumla unanufaika na raslimali zao.
3.1.3 CHADEMA inaamini katika kujenga na kuimarisha uchumi wa soko huru, utakaoheshimu na kulinda haki na mali za watu, biashara huru na sekta [COLOR=#009900 !important]ya[/COLOR] watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyeti hususani pale penye hitilafu ya soko au penye maeneo nyeti ya kiuchumi. Tunaamini katika soko huru sio soko holela.
3.1.4 CHADEMA inaamini kuhakikisha matumizi [COLOR=#009900 !important]bora[/COLOR] ya raslimali asilia za nchi ili zichangie kikamilifu katika pato la taifa na hasa kuboresha huduma za kiuchumi zinazotumiwa na wananchi wote.
3.1.5 CHADEMA inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi zetu zilizo nzuri.
3.1.6 CHADEMA inaamini katika uhuru chini ya sheria zilizo za haki.
3.1.7 CHADEMA inaamini katika siasa ambazo ziko juu ya vyama zenye kusimamia zaidi maslahi ya Taifa.
3.1.8 CHADEMA inaweka umuhimu wa pekee katika familia kama moja ya taasisi muhimu ya kijamii.
3.1.9 CHADEMA inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya dola.
3.1.10 CHADEMA inaamini taifa linaundwa na watu, hivyo uhai wake unawategemea watu, na mabadiliko yake yanatokana na watu.
3.1.11 CHADEMA inaamini katika kujenga uwezo wa wazawa katika kumiliki na kuendesha uchumi.
3.1.12 CHADEMA inaamini kumiliki raslimali na mali miongoni mwa wananchi kunawapa uhuru zaidi hivyo tunataka kujenga chama na baadaye taifa lenye kutoa fursa, ambapo kila mtu bila kujali asili na hali yake anaweza kutimiza na kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake.



[/COLOR]


 
Kwanza CCM Ing`oke ndo mpango mzima By Prof: Lipumba
 
naomba nikufundishe kitu, sera za chadema hazipo kwenye makaratasi tu, na kama zingekuwa kwenye karasi tu basi hiko kisingekuwa chama cha siasa kinachotaka kuwaongoza wananchi wake kupata maendeleo. bali sera ya kwenye karatasi inahitaji utekelezaji na ndo maana tunapiga vita ufisadi kwa hiyo hatuwezi kuacha lkusema pale inapotokea eti kwa kuwa sera ipo. hivi kwa mfano ubadhirifu uliofanywa na serikali ya ccm pale mwanza tusiseme kwa kuwa tutakuwa tunakwenda na matukio? pole kwa kuwa najua inawezekana haukuelewa umeandika nini. lakini pia siku nyingine usipokuwa na jambo la kusema ni bora ukae kimya.
 
Back
Top Bottom