Hivi mawaziri waliodaiwa kujiuzulu wasipofanya hivyo tutafanyaje? Tusaidiane mawazo

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
Chama Cha Mapinduzi kinasifika kwa sera za kulindana maarufu kama mwenzetu. Hali ilivyo ni kwamba ule moto wa jana wa 'kujiuzulu' saba unaendelea kuzimika. Je ikitokea jamaa wakafanya kama walivyozoea, kulindana, kama watanzania tutafanya nini?Je bunge letu litakuwa na heshima tena? Je tutavumilia au kwenda Taharir kama wenzetu wa Misri ambao wamerejea uwanjani kuhakikisha serikali ya kijeshi inaondoka?
 
Sisi watanzania tunafika mahali tunafanana na wabunge waa ccm tu kulalamika na kutoa mishipa ya shingo na mapovu bila kuchukua hatua! rais, wabunge , mawaziri watumishi wote wa umma sisi ndio maboss wao kwa mujibu wa katiba ibara ya 8 sasa kama hawatendi tunavotaka kwa nini tuwabembeleze kujiuzulu? Tuingieni barabarani tuwatoe kwa nguvu! tuunge mkono juhudi za vijana wetu akina zitto kwa vitendo au tukae kimya nchi iendelee kuliwa na sisi tuendelee kuwa maskini hakuna haja kulalamika tena tuchukue hatua tupangilie maandamano makubwa nchi nzima hadi waondoke na wafikishwe mahakamni wafilisiwe au tukae kimya tusiwe kama akina godfrey zambi kelele nyingi kusaini order paper ya zitto hawataki!!
 
Bwana mpayukaji!
Me nadhani huu ndo mtaji wa cdm, kwani kuto wajibika kwao kunatoa fursa ya wana cdm kuwa na nguvu zaidi za kisera na hata kukubalika.
 
Back
Top Bottom