Hivi kwanini Wazungu huchangamkiwa sana kwenye maofisi kuliko sisi Wabongo?

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Utakuta ukiwa ofisi fulani unadharaulika sana na kupigwa danadana kibao kupata huduma.
Sasa aje mzungu, utaona wenye ofisi wanavyobabaika kumchangamkia na kujitabasamisha na broken kibao!

Nimejiuliza hali hii ni Colonial hangover, kutojiamini, kujipendekeza au ulimbukeni?!

Huko kwao hutakaa ukutane na huu upuuzi.
 
Sijui ni ujinga au uoga hata sielewi, yaani mtu akiona mzungu anachanganyikiwa na hii ndio iliyopelekea UDSM kuingizwa mkenge na yule mwekezaji pale Mlimani city, pamoja na lundo la wasomi waliojazana pale.
 
Utakuta ukiwa ofisi fulani unadharaulika sana na kupigwa danadana kibao kupata huduma.
Sasa aje mzungu, utaona wenye ofisi wanavyobabaika kumchangamkia na kujitabasamisha na broken kibao!

Nimejiuliza hali hii ni Colonial hangover, kutojiamini, kujipendekeza au ulimbukeni?!

Huko kwao hutakaa ukutane na huu upuuzi.
Tanguliza neno ,vip MBONA mmepoa sana jamani, kuna nn? hamjapata Chai kamateni hii angalau soda,then utapata hilo tabasamu na uchangamfu uutakao.Mimi nikienda ofisi huwa nafata huduma sijafata tabasamu au uchangamfu,maadam nikitakacho tapata hata ukiwa bubu sijali.
 
Wanatoaga tip nzuri.. Hata wewe ukijijengea utaratibu wa kutoa tip lazima utachangamkiwa..
Si utafilisika, kuanzia mapokezi mpaka uje ukutane na afisa mhusika wa shida yako, utatoa kiasi gani? Na ni kila ofisi/ taasisi!
 
Zamani wakati nataka Kupiga customer service / care mtandao wa vodacom na switch to English, haiiti zaidi ya dakika mbili tayari attendant kashaidaka ila uki switch kiswahili utawekewa series za kikorea mpaka sikio livuje damu
ivi nikiamua kuswitch english then ikapokelewa na nikaongea kiswahili je sitahudumiwa?????
 
Zamani wakati nataka Kupiga customer service / care mtandao wa vodacom na switch to English, haiiti zaidi ya dakika mbili tayari attendant kashaidaka ila uki switch kiswahili utawekewa series za kikorea mpaka sikio livuje damu
Kwakwaaakwaaaa...Haki umenichekesha sana! :D:D:D
 
Wepi hao watoa tip hao waliochoka hakuna Mzungu awezae nunua haki yake,kama kila kitu kakamilisha atakwambia for what?
Tip sio rushwa,tip ni appreciation (asante)
Wenzio wana lamba tip anza na wewe kutabasamu na kuchanyamkia kila mzungu au mtu yeyote yule ili ulambe tip.
 
Back
Top Bottom