Hivi kwanini viongozi wanapostaafu uwaziri wanageuka mbogo kwa serikali iliyopo madarakani?

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,982
45,897
Nataka kujua tu huko kuna nini mpaka kiongozi yoyote anapotoka katika nafasi ya uwaziri anakuwa mkali kweli kweli na serikali iliyopo madarakani.

Wapo wanaoikosoa wazi wazi, ila wapo waliokwenda mbele na kugombea urais kabisa vyama vya upinzani. Mifano hao ya waliovuka mipaka mpaka kugombea nafasi upinzani ni Lowasa na Sumaye hawa walikuwa mawaziri ila baada ya kutengwa walikuwa wakali kweli kweli na kuamua kujitenga kabisa na kundi walilozoea kuwemo.

Sio hapa nchini tu, ila huko duniani pia mifano ya mawaziri kuja kuwa wagombea Urais, au kupinga serikali baada ya kutolewa katika nafasi hiyo ni mingi sana. Na inatokea mara kwa mara.

Nafasi ya uwaziri, ina nini mpaka kila anayeondolewa au kustaafu, lazima awe mkali kweli kweli.
 
Kwanza ni unafiki waliokuwa wanaufanya wakiwa madarakani kwamba hawaguswi na hustle yoyote. Sasa huku site ni tofauti na kule. Stress kibao huku. Pili, viongozi wote wakitoka madarakani busara na ubinadamu vinaongezeka, hasa viongozi wa kiafrika. Sasa wanaona wanachotendewa wao na wananchi wanaoishi nao siyo haki
 
_20170518_081854.JPG
_20170518_110301.JPG
_20170518_110243.JPG

Mmoja wapo
 
Wanapokuwa mawaziri inaonekana wanabanwa na collective responsibility, na wanakuwa upande wa serikali.
Ila tungewaelewa vizuri kama wangeresign uwaziri kwa sababu maoni yao mazuri wanayoyatoa sasa hayakusikilizwa. Cha ajabu ukiwapa tena uwaziri huta kaa uwasikie tena...
Ndio maana unashindwa kujua Nani hasa anauchungu na taifa Lake na anaonyesha consistency
 
Nataka kujua tu huko kuna nini mpaka kiongozi yoyote anapotoka katika nafasi ya uwaziri anakuwa mkali kweli kweli na serikali iliyopo madarakani.

Wapo wanaoikosoa wazi wazi, ila wapo waliokwenda mbele na kugombea urais kabisa vyama vya upinzani. Mifano hao ya waliovuka mipaka mpaka kugombea nafasi upinzani ni Lowasa na Sumaye hawa walikuwa mawaziri ila baada ya kutengwa walikuwa wakali kweli kweli na kuamua kujitenga kabisa na kundi walilozoea kuwemo.

Sio hapa nchini tu, ila huko duniani pia mifano ya mawaziri kuja kuwa wagombea Urais, au kupinga serikali baada ya kutolewa katika nafasi hiyo ni mingi sana. Na inatokea mara kwa mara.

Nafasi ya uwaziri, ina nini mpaka kila anayeondolewa au kustaafu, lazima awe mkali kweli kweli.

Kwenye bold,una uhakika au hujui lugha ya kiswahili vizuri?
1.Pinda
2.Mungai
3.Warioba
 
Wengi wao huwa wana mindset za kimasikini na hujiona wameukata wawapo madarakani. Huko kwenye uwaziri huwa wanaishi maisha yasiyo halisi kwani hupata mshahara mnono na marupurupu kibao ambayo hawana uwezo waka akili ya kuzalisha pindi watokapo madarakani na wakati huohuo wakipewa heshima za kinafiki na kujiona wao ni miungu watu. Wanapotoka madarakani hayo yote hupotea na kurudi kwenye maisha yao halisi. Hapo ndio huona mapungufu ya serekali ambayo walikuwa vipofu walipokuwa ndani. Matokeo yake ni kuwa wakali ili kuifanya serekali hiyo hiyo inayoongozwa kinafiki iwaogope kwani wote wanajuana kwa unafiki wao.
 
Na huyu alichangia mambo mengi mabaya na ya kihunihuni tu kama kufuta bunge live na sheria ya uhalifu wa mitandaoni na kuminywa kwa uhuru wa habari kwa ujumla. He was high and now is sober.
Dhambi inamtafuna hiyo
 
Wanapokuwa mawaziri inaonekana wanabanwa na collective responsibility, na wanakuwa upande wa serikali.
Ila tungewaelewa vizuri kama wangeresign uwaziri kwa sababu maoni yao mazuri wanayoyatoa sasa hayakusikilizwa. Cha ajabu ukiwapa tena uwaziri huta kaa uwasikie tena...
Ndio maana unashindwa kujua Nani hasa anauchungu na taifa Lake na anaonyesha consistency
Kwa maana hiyo Mbowe akiteuliwa kuwa waziri, atamsuport Rais, ila akienguliwa anarudi kule kule?
 
Back
Top Bottom