Hivi kwanini Beno Ndulu hawajibishwi?

jembepori

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
618
193
Niliwahi kuhudhuria warsha moja ya Repoa mwaka 2007 na mzungumzaji mkuu alikuwa ni Beno ndulu....alipo simama kuongea akatoa takwimu jinsi sekta mbalimbali zinavyochangia kwenye ukuaji wa uchumi.....eti akasema sekta ya madini inachangia 3% tu kwenye ukuaji huku sekta ya usafirishaji ikiongoza kuchangia kwenye uchumi wa nchi......palepale nilijua kunashida mahala na ndipo nilipodharau uprofesa wake.....nilijiuliza maswali mengisana hasa kulingana na elimu yake kulinganisha na manenoyake........kwakweli tangu sikuile nilipoteza imani na huyu gavana wetu...........leo rais kanisaidia kuthibitisha kile nilichokuwa nakiwaza bila kumshirikisha mtu.....kumbe hata takwimu zenyewe za madini huwa hatunzi....inaeleke hatazile alizotutajia sikuile usikute ni za kufirikirika tuuu!.. Hajatajwa kwenye majina yale rais aliyoyabariki kuhojiwa.....ila swalilangu kwani yeye kwa hapa alipo tufikisha hivi hatakiwi kuwajibika kweli?.......mimi Ninahakika hata rais alitamani kumsimamisha kazi ila kwa sababu na yeye anadamu kutokana na simamishasimamisha zilizopita alijirudi tu maana watu watasema sana........utasikia"hivi kwani kila hotuba ni lazima atumbue.....hizi sasa ni sifa".. Najaribu tu kufikiri kwa sauti....Iakini ukweli ni kwamba mheshimiwa rais we chapa Kazi...hii nchi inauozo wa kutosha na huku mtaani sisi tumeshakuelewa.....wale wa mkate na blueband hawatakaa waje kukuelewa ila sisi mihogo ya kukaanga na maji tunakuelewa....tukonyumayako na tafadhali tunakuomba utusafushie na mfumo wa Benki kuu yetu kwa kumwajibisha huyo bosi mkubwa.....nchi hii ni yetu Sote na mtu unapofanya ubaya huwa unajua sema tu wakati wa kuwajibishwa utajitutumua kwa nje kusema na kulalama kuficha aibu lakini ndani ya roho yako huwa unashuhudiwa kwamba you diserve it.......Mungu akupe nguvu ya kuirekebisha nchi hii ya Mungu sir....

Mungu Ibariki Tanzania
 
Prof. Ndulu hawezi kudumu pale, si umsikia Rais amesema kuna PhD 17 BOT lakini hamna kitu. Pia juzi juzi tu hapa amepeleka manaibu Gavana wawili moja wapo ni Mchumi Msomi Dr. Yamungu aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi. Unganisha nukta hizo.
 
Je waziri wa viwanda na biashara (BRELA) Mh. Charles Mwijage atapona kutokana na ACACIA ''kukosa'' leseni ya usajili wa Kampuni ?

Mwijage, Kinana waielezea Ripoti ya Pili iliyokabidhiwa kwa JPM

Source: Millard Ayo
 
Nasubiri watu watakapomwaga mboga na ugali, ila sizani kama hii stage itafika maana watamwambia boss mbona kwenye vikao vyote ulikuwepo hivyo unawajua wezi vizuri, maana wenzake wanajua kabisa kile anachokifanya ni maigizo.
 
Ripoti ya pili ya Madini Wachambuzi wataalamu waja na Maoni Tofauti :
  1. kusajiliwa au kutosajiliwa Kampuni ya ACACIA
  2. kubadilika majina kufuatana na sheria za Tanzania
  3. kuendesha kampuni ''kinyume'' na sheria za uendeshaji kampuni Tanzania
  4. kupanga kodi au kukwepa kodi kufuatana na sheria za kodi za Tanzania Revenue Authority
  5. BoT taarifa ya February 2017 inaonesha mchango wa dhahabu ktk uchumi wa Tanzania 2% tofauti na ''kukosekana'' taarifa ya '' a gold reverse'' a.k.a akiba ya ''vitofali vya dhahabu'' badala ya akiba za fedha ktk dollar, rand, Euro n.k za miezi mitatu
  6. Uwoga, usiri wa mikataba


Source: Bin Seif
 
Mbunge William Ngeleja ajitetea Baada ya Ripoti ya 2 Madini Kuwataja Mawaziri wa Zamani


Source: Bin Seif
 
Kumshitaki Beno ni ngumu kama ilivyokuwa ngumu kumshitaki Daud Balali, kuna mazabazabe mengi ya magamba amewapitishia anayajua kwa vimemo vyao yeye sio mjinga anajua yaliomkuta Balali
 
Huyu gavana kajitahidi lakini anafanya kazi chini ya maamuzi ya siasa hata akiletwa gavana mwingine hakutakuwa na mabadiliko
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom