Akili Unazo!
JF-Expert Member
- Feb 18, 2009
- 3,930
- 4,893
Mzee, kitchen party ni unyago mamboleo kwa wamama. Ni mafundisho ya jinsi ya kutunza mume na nyumba ya ndoa. Mafunzo haya yanaweza kurudiwa kwa vipindi kadha wa kadha kama refresher course. Ndo maana unakuta hata wale waliokwishaolewa wanaweza kurudi tena kukumbushwa au kufundwa mapya ambayo sayansi na teknolojia imeyavumbua. Yapo mazuri mengi huko kwenye KP lakini pia kuna mikengeuko ya aina yake. Yategemea walimu wao kwani si wote ni wazuri.
msitari wa mwisho wa hoja yake anasema kuwa, (namnunkuu) "Wakuu nisaidieni maana yake naweza nisisfanyiwe kitchen party siku nikipata mwenza"
Kwa kuzingatia hilo, naomba usimwite mzee, kama nilivyokusoma kwenye hiyo nyekundu, usije ukamkosesha mchumba mwenzio buuuuuuure, mwaya!
Sherehe ya jikoni!!
Babuyao kakujibu vema chaku
Jamani nilikuwa najua siku zote Chaku ni mwanaume sorry for that chaku sasa nimeelewa.
Wakuu nimekuwa nikisikia dada zangu wakifanyiwa kitchen party pale tu wanapokaribia kuolewa hata kwa yule aliyekwisha zaa anapofika hatua ya kubariki ndoa yake anafanyiwa kitchen party.Sasa swali Huyu ambaye alishaolewa bila harusi kitchen party ya nini?
Je kama kwenye kitchen party wanafundishwa maadili ya kumheshimu mume wake mbona wakiolewa wanayasahaho yote bila hata kuyafuata walioambiwa na waliowafanyia kitchen party?
Kitchen Party ni utamaduni wetu au umeigwa kwenye mitandao.
Wakuu nisaidieni maana yake naweza nisisfanyiwe kitchen party siku nikipata mwenza.
Kitchen Parties zimeshika kasi.....hata mashankupe, mashangingi, maveterani yanayojua A to Z and beyond eti yanafanyiwa kitchen party yakiwa yanaolewa!!! nafikiri imekaa kibiashara zaidi=kukusanya zawadi kwa binti/mama/muolewaji. nimejaribu kuhesabu ndoa za marafiki zangu za hivi karibuni...nimegundua zaidi ya nusu zimesambaratika====nafasi ya kitchen ipo wapi?
kuna mama mmoja maarufu sana wa kusherehesha hizo kitchen party Dar,yeye hajaolewa na ana watoto wawili kila mmoja na baba yake,i fail to imagine anafundisha nini kwa maneno na matendo kama si 'akikuzingua rudi nyumbani?'.
siku hizi kuna matangazo lukuki kwenye media yanayoitwa 'VUNJA UKIMYA', je sasa serikali ime-admit mafundisho ya ndoa hakuna hadi watu wa marekani wanatufunda? maana mwisho wa matangazo utasikia 'tangazo hili limewajia kwa hisani ya watu wa marekani'.
.................i submit...........
hehehehehe nimeipenda hiyo hapo kwenye red.mwingine anafanya hiyo sijui ndo sherehe ya jikoni, then haolewi wala nini, kibiashara zaidi.