Hivi huwa mnashangaa nini?

that manzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
386
Reaction score
1,247
Habari za jumapili wana jf,

naomba kuwauliza wenye magari yenu hivi mkiwa mnapita kwenye vituo mkakuta watu wamesimama huwa mnagueza shingo zenu kushangaa nini?

mnahisi kuna watu mnawajua?
mnaangalia kama kuna watu mnaweza kuwapa lift?
au mnatushangaaa kwanini hatuna magari? au tunaonekana mga kama vikatuni😂

mje mnijibu😂
 
Tunawashangaa waisraeli hapo kituoni...miaka 40 kwa mguu😁
 
Tunataka kuona kama mnetuona na kama ilikuwa bado basi mjue kuwa ni mimi nimepita
 
Hahahahaaa, tunajiuliza tusimsme tuwasalimie ile kijapan kiheshima kama 'namaste' au tupige honi tu.

Tunachagua honi, lakini tena tunaanza kuwaza je wakihisi nnawapigia kelele, au nataka abiria??😆🤫

mara shwaah tushafika mbali na haijalishi tena tutachagua kipi, ndo tushachelewa aaaaaaargh!
 
Wewe kwanini unashangaa gari la mtu, mpaka unajua amegeuza shingo, kwanini unashangaa gari lake?
Unahisi unamjua dereva? Au unaangalia kama anaweza kukupa lift?
Au unashangaa kwanini anamiliki gari?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…