Hivi hata kuchat na mwanamke siku hizi ni mpaka utoe takrima?

Kakole

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,094
1,745
Happy new year to all.
natumai wote mko fresh na mmeanza mwaka vyema, tushaingia mwenzi mgumu wa January watu tumeenjoy sikukuu zote sasa vichwa vishaanza kuuma ada za shule na mambo mengine kibao.

anyway bila kuwapotezea mda, kulingana na kichwa cha habari hapo juu, nashindwa kuelewa nini kinaendelea ktk kipindi hiki maana kila nikichat na mdada tu napigwa mzinga wa hela, sasa mimi nashindwa kuelewa kuwa kwani siku hizi kuchat na mtu wa jinsia tofauti hasa wanawake ni mpaka utoe takrima? hatuwezi tu kusalimiana na kujuliana hali ikaisha bila kulia shida? hali hii ikiendelea basi itafikia hatua watu tutakuwa hatusalimiani kwakweli.
 
Ila tunaenda sambamba bana, kuna wanaume wanaomba hela mweh! Yani kuna watu wawili katika phonebook yangu tena ni wanaume yani wanaomba hela jamani utadhani mi ni mwanaume nachefukwaga hawajui tu
Utakua umewazidi akili na uwezo that's why
 
Ila tunaenda sambamba bana, kuna wanaume wanaomba hela mweh! Yani kuna watu wawili katika phonebook yangu tena ni wanaume yani wanaomba hela jamani utadhani mi ni mwanaume nachefukwaga hawajui tu[/QUOTE

He he he mjini kina Mario wanaongezeka kila kukicha, wanaume km wanawake we acha tu nisichonge sana
 
Hapo wana test ili ukiingia wajue una uwezo wa kumfanya aishi town,Hivi vitu vina Tegemea na umri na kipato mkuu hata Mimi zamani nilikuwa naomba vocha,baadaye ni nunulie nguo,Viatu then ikaja kodi ya nyumba hivi sasa ni Gari
 
Back
Top Bottom