Hivi Google wanalipa kodi Tanzania?

Secret Star

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
1,720
1,639
Jamani sio siri tumekabwa kwenye kulipa Kodi! hakuna tena njia ya panya ya kukimbilia ama kujificha.

Si jambo baya sana, ila selikari inatakiwa kutulegezea kidogo wananchi wa hali ya chini ili walao tuone ahueni kidogo ya maìsha, sio kila siku tuone Afadhari ya mwaka jana au mwaka Juzi.

Nina Swali kidogo ambalo linanipa mashaka, na nikiwa kama raia napaswa kujua hili. Ni kuhusu Makampuni makubwa ya kimataifa ya mtandao wa Internet kama Google, na Mitandao mingine mikubwa Duniani kama vile Facebook, Yahoo, Twitter na mingineyo inayotembelewa na mamilioni ya watanzania kila siku.

Swali ni JE GOOGLE na FACEBOOK WANALIPA KODI TANZANIA?
Kampuni kama Google na Facebook hapa Tanzania ni moja ya makampuni yaliyoshika mno Raia kupitia Simu zao, Android, Mtandao wa Video Youtube, Google search Engine, Whatsapp, Instagram, Google Chrome browser na mamia ya huduma zao zinazopitiwa mno kila siku hapa Tanzania kwa Pesa zetu sisi walipaji kodi sugu.

Swali ni je Kampuni hizi zinalipa kodi Tanzania? na kama zinalipa Kodi nahitaji kujua Ulipaji wake Ukoje na Kampuni hizi zimeilipa Tanzania Kiasi gani Tangu zilipoanzishwa mpaka sasa?

Pia nahitaji kujua Kama zinatakiwa kulipa ni Kampuni Gani zilizoshindwa kulipa Kodi na zimefungiwa hapa Tanzania kwa malimbikizo ya Madeni ya kodi?
Wote Tunatambua Wamiliki wa makampuni haya ni matajiri wazito Ulimwenguni kama Mmiliki wa Facebook ambaye anamiliki zaidi ya Trioni 99 za Kitanzania mfukoni Mwake kwa pesa tunazompa sisi kila siku na Wengine wengi.

MAKAMPUNI MAKUBWA YA MTANDAO WA INTERNET YA NJE YANALIPA KODI TANZANIA?

Nawasilisha.

Secret Star//
 
Badala ya kuwa charge hayo makampuni utasikia wanaanza ku-charge wanaotembelea mitandao hiyo wakiwa Tanzania!!
Yah, Makampuni ya Simu na Raia tunalipa kodi kisawasawa hakuna njia ya panya ila sijui kama Facebook wanalipa mapato Tanzania
 
walipe kodi kwan wamesajiliwa Tz, au wana ofisi yoyote Tz?

Nadhani users wengi wa Tz wanaitumie hiyo mitandao kama service only so Google hawahitaji kufungua ofisi Tz, ila kama makampuni makubwa yataanza kutumia service za Google/Youtube/facebook then itawalazimu kufungua ofisi Tz na hapo ndipo watakapolazimishwa kulipa kodi otherwise waache waendelee kutubeba beba
 
Suala la wao kutokuwa na ofisi si shida ilihali kazi yao inafika Tanzania, hili jambo nadhani linatakiwa kuangaliwa vizuri.
 
Ni sawa na kuuliza hivi zile channel za mpira online au kideoni je zinalipa kodi Tanzania?kwanza utazikamatia wapi,labda izimwe internet,(napo utakua wa kwanza kulalamika na maandamano juu)kodi inalipwa na wenye kutoa huduma ya internet(kwa kuunga bando) vingamuzi Tz baada ya wao kununua channel hizo.
 
Mfumo wa Chanel za Tv sina uhakika kama hawalipi Kodi mfano DSTV ni watoto wa DSTV ambapo DSTV nadhani wanalipa Kodi Tz, Vipi kuhusu Facebook?
 
Back
Top Bottom