Hivi Escrow ni Ufisadi au Promotion?

 
Hivi yule jamaa wa signature ya "SYSTEM AT WORK" bado yupo? Natumia Simu, sioni baadhi ya mambo
 
Unatarajia mnazi wa ccm na yule wa chadema(ukawa) wakupe majibu ya aina gani hapa? Nadhani WAZALENDO wachache sana waliobakia ktk nchi hii wataishia kusoma post yako tu na hawatatoa coment yyt ile, sio kwasababu hawana majibu au hoja la hasha!~ ni mtazamo wangu tu lkn.
 
JK alishasema, pesa za ESCROW si za UMMA. Kwa maana Rugemalila aliamua kugawa pesa zake baada ya kuwa na ziada kubwa katika utajiri wake.

Sijui kwa nini walalamikaji kuhusu Escrow acc wanasahau hitimisho hili muhimu. Serikali ilishasema hizo hazikuwa pesa zake bali za wanahisa wa IPTL (wafanyabiashara binafsi). Tibaijuka na wengine hawakuwajibishwa kwa makosa ya jinai kuhusiana na Escrow bali kwa kutotoa taarifa mapema kuhusu kupokea kiasi kikubwa cha pesa kulingana na kanuni za maadili ya viongozi serikalini.

Kwa msimamo huo wa serikali ambao haujabatilishwa na mahakama, ni kupoteza muda kuwazungumzia wahusika wa Escrow acc kama mafisadi au wajinai (criminals). Ni vyema mjadala ujikite kuhusu busara nzima ya kuwa na uwekezaji wa aina ya IPTL na namna ya kuachana na aibu/hasara hiyo kwa taifa. Someni makala za Mihangwa kwenye Raia Mwema.
 
Mrudisheni na werema basi , mbona mmemtenga ?
 

Kama Escrow ilikuwa Mali ya wanahisa a.k.a wawekezaji binafsi, ilikuwaje ikatunzwa BOT?, siku hizi BOT wanatunza pesa binafsi? Kama pesa si ya Umma nini hasa dhima ya maelekezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye pesa ambayo inawahusu watu binafsi? Nini hasa ilikuwa nia na lengo la Gavana wa Benki Kuu kutaka Mwongozo toka Serikalini juu la kulipa Fedha za Escrow ambazo wana sema ni Mali binafsi? Tangu lini Fedha za mtu binafsi zikaombewa mwongozo Serikalini?

Tukubali tukatae Escrow Acc ilikuwa na Fedha za walipa Kodi wa Tanzania.
 

Mkuu sikubishii unachosema. Lengo langu ni kusisitiza msimamo iliotoa serikali kuhusu suala hili na kutaka tuufanyie kazi badala ya kuhangaika na watu binafsi kama Muhongo na Maswi ambao walikuwa "wakitumwa" tu kufanikisha ulaji wa "wenyewe". Hao "wenyewe" ndio waliotufunga na mkataba wa ovyo sana wa IPTL ambao unaendelea kufilisi taifa kupitia TANESCO (soma makala za Mihangwa katika Raia Mwema). Usifikiri ulaji kupitia IPTL ulianza na kuishia na acc ya Escrow. Zaidi ya pesa za Escrow acc, kila mwezi TANESCO inailipa IPTL kama USD 4m za "capacity charges". Jiulize wanufaika wa malipo hayo ni kina nani hasa na kwa nini tunaendelea kuendekeza mkataba wa aina hiyo. Badala yake naona watu wameng'ang'ania kupambana na akina Muhongo badala ya wahusika "wenyewe".
 
Nimekuelewa mkuu, hao wahusika sasa ndio tunawataka haswaa, hayo ndio majipu ya kutumbua tunayoyataka. Hatutaki dilly dally za kuhangaika na vipele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…