Hivi CCM wanaeeza kuleta mabadiliko gani? Tuwaeleweje?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,252
8,003
Yaani wabunge wa CCM pamoja na mwenyekiti wao wa chama wamekua bungeni miaka yote ndani ya bunge na kutunga sheria kwa kuziunga mkono kwa kura zao wenyewe na wingi wao, ati watuletee mabadiliko kweli? Inawezekanaje leo. wakane visheria vyao waliokua wakivipitisha bungeni?

Mtukufu wetu nae alikuwepo bungeni miaka yote 20 ya ubunge wake ni kwanini asingesisima imara kama mwanaCCM ajitofautishe na wanaccm wenzake kwa kukataa haya ambayo anapigana nayo hivi sasa pengine umma ungeweza kumwelewa hivi sasa kwa kila anachokisena?Hivi utamwaminije mtu anayekataa mboga aliyoipika yeye kwa kukwambia kua sio nzuri? Kwanini usiamini kua anataka kukudangaya?

Hivi ni kweli ndio leo CCM wanashtuka? Kuthibitisha kua hawawezi kufanya chochote mpaka kufikia 2020 tazameni hali ilivyo hivi sana pamoja muda kuyoyoma. Kila kukicha ni uteuzi na utenguzi, sasa kama ni hivyo inamaana tu kupitia zoezi hilo inaonesha kua hakuna anayemwamini mwenzake hivi sasa,kama hakuna kuamimiana utezi huu na utenguzi hadi lini angalao tukae tulijenge taifa? Nijuavyo mimi malaika ndio wakamilifu peke yao na sio wanadamu!

Ndugu yangu Pole pole anataka kujiuma mdomo waziwazi kujaribu namna ya kukwepa kuzungumzia suala la kukumbatia mtu asiye na vyeti, mpaka anatia huruma na aibu.
Mpaka hapa suala la vyeti linaiporomosha CCM tu na sisi raia wema hatutakubali kamwe mpaka mtu huyo atakapoachia ngazi yeye mwenyewe na sio mpaka afukazwe.Tatizo sio madawa ya kulevya kama inavyopotoshwa,tatizo vyeti feki.Toa vyeti vyako halali. endelea na kazi zako.


Inatafutwa kila namna ya kumtetea mhalifu wa vyeti lakini bado aibu na Roho wa Mungu anawaumbua. Mungu hua hadhihakiwi, Mungu husikiliza vilio vya waja wake kuliko vitisho kutoka kwa watu wachache.Haiwezekani mtu anatetea haki za Wanyonge anasimama wewe unanyooshea silaha ya moto kumtishia kuutoa uhai wake! Hakika katika hili Mungu atanyoosha iko siku tutazungumza.

Hakuna mwananchi sasahivi anaweza kuizungumza CCM, kama mtu anataka kulithibitisha hilo naomba ianzishwe operation kama ilivyokua ya kinana na Mh Nape tuone watu watakavyozomewa.
 
Wameshia kuwa wa watu wa kuteua na kufukuzana. Sasa sijui watapata wapi muda wa kuwaletea watanzania maendeleo kama wao wapo busy kwenye tafrija za kuapishana huko ikulu.
 
Back
Top Bottom