Hivi binadamu hutimiza meno 32 akiwa na miaka mingapi?

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
8,288
Reaction score
18,579
Mnaopenda salamu leo siwasalimii, msiizoee salamu yangu....

By the way nina swali dogo tu nataka kukuulizeni, hivi mtu huwa na meno 32 akiwa na miaka mingapi? Maana kila nikihesabu meno naona hayajatimia 32, yapo 28 ina maana bado yanapelea manne. Mwanzo nilikuwa nahesabu kwa kutumia ulimi nikaona kama ulimi unanidanganya nikaamua kuhesabu kwa kutumia kidole lakini hesabu ikabaki ile ile, 28.

Inafika mahali sicheki kwa amani maana kuna msemo wa wahenga unasema "anacheka hadi meno yote 32 yanaonekana", sasa mimi nina hofu kuwa nikicheka sana watu watahesabu meno yangu na watagundua kuwa hayajatimia 32 jambo ambalo litanisababishia aibu na fedheha kubwa kwani nitaonekana mimi siyo mtu mzima bado.

Na kila nikipitisha ulimi kwenye fizi ili nione kama yataota hivi karibuni, wala hakuna dalili, hata nafasi iliyobaki ni ndogo mno, haitoshi meno yaliyobaki kuota. Hii hali inanitia wasiwasi sana.

Enyi wenye meno 32 tayari, kwani yalifika idadi hiyo mlipokuwa na miaka mingapi? Tupeane uzoefu.

NB: kuna watu watakuja na maneno ya kejeli kuwa 'wenzako wanahesabu pesa wewe una hesabu meno!' Kila mtu ahesabu alichonacho.
 
Wewe subiri utakapokuwa mkubwa meno hayo yataota tu, kwanini unataka kumshurutisha Mungu aliyekuumba!!, hayo meno mengine uliyonayo yalikujaje???, au umeshindwa kutafuna nyama??, vuta subira dogo hadi upevuke.🤣
 
Mnaopenda salamu leo siwasalimii, msiizoee salamu yangu....

By the way nina swali dogo tu nataka kukuulizeni, hivi mtu huwa na meno 32 akiwa na miaka mingapi? Maana kila nikihesabu meno naona hayajatimia 32, yapo 28 ina maana bado yanapelea manne. Mwanzo nilikuwa nahesabu kwa kutumia ulimi nikaona kama ulimi unanidanganya nikaamua kuhesabu kwa kutumia kidole lakini hesabu ikabaki ile ile, 28.

Inafika mahali sicheki kwa amani maana kuna msemo wa wahenga unasema "anacheka hadi meno yote 32 yanaonekana", sasa mimi nina hofu kuwa nikicheka sana watu watahesabu meno yangu na watagundua kuwa hayajatimia 32 jambo ambalo litanisababishia aibu na fedheha kubwa kwani nitaonekana mimi siyo mtu mzima bado.

Na kila nikipitisha ulimi kwenye fizi ili nione kama yataota hivi karibuni, wala hakuna dalili, hata nafasi iliyobaki ni ndogo mno, haitoshi meno yaliyobaki kuota. Hii hali inanitia wasiwasi sana.

Enyi wenye meno 32 tayari, kwani yalifika idadi hiyo mlipokuwa na miaka mingapi? Tupeane uzoefu.

NB: kuna watu watakuja na maneno ya kejeli kuwa 'wenzako wanahesabu pesa wewe una hesabu meno!' Kila mtu ahesabu alichonacho.

Ngoja nikusaidie dogo, meno hayo yanayoitwa kwa jina jingine "wisdom teeth" huota katika umri wa kati ya miaka 17---25, lakini wengine huchelewa kuota hata zaidi ya miaka 25.

Kwa maelezo zaidi muone/consult daktari wa meno (dentist).

Safi dogo, ✊🏻
 
Hizo wisdom teeth zikiota vibaya cha moto chake ni kikubwa kuliko jino lililotoboka
 
Mtu unakuwa na meno 28 + 4 wisdom teeth, afu nasikiaga hizo eti sio kwa wote zinaweza kumalizika kuota na wengine zikaota kwa kuchelewa. Binafsi mpaka dk hii ninayo 30 kwa ujumla wake na wisdom nilishatoa moja.

Ningekuwa sijatoa sahii ningekuwa na 31 😀

Uking'oa wisdom tooth na wisdom yako inapungua pia.
 
😂😂😂mimi yale magego ndio yanachomoza fizi zinaumaje, hauko peke yako
Haya meno ni miyeyusho sana, mimi kuna wakati fizi zinauma kweli kweli najua hapa tayari show inakaribia kwisha, lakini baads ya siku kadhaa, kimyaaa.....
Sasa ipo siku nitayagongagonga nitayagongagonga hadi yakate tamaa.
 
Ngoja nikusaidie dogo, meno hayo yanayoitwa kwa jina jingine "wisdom teeth" huota katika umri wa kati ya miaka 17---25, lakini wengine huchelewa kuota hata zaidi ya miaka 25.

Kwa maelezo zaidi muone/consult daktari wa meno (dentist).

Safi dogo, ✊🏻
Unaona sasa, tayari watu mmeanza kuniita dogo kisa tu mmeshajia nina upungufu wa meno manne....

Ila mkuu shukran kwa ushauri wako. Nitaufanyia kazi.
 
Mtu unakuwa na meno 28 + 4 wisdom teeth, afu nasikiaga hizo eti sio kwa wote zinaweza kumalizika kuota na wengine zikaota kwa kuchelewa. Binafsi mpaka dk hii ninayo 30 kwa ujumla wake na wisdom nilishatoa moja.

Ningekuwa sijatoa sahii ningekuwa na 31 😀
Kumbe yana na jina kabisa...nilikuwa sijui aisee😀😀😀

Kwa hiyo mkuu kwa sasa piga ua huwezi kufikisha 32, pole sana mkuu... kama yangekuwa yanakodishika ama kukopeshwa ungeongea na mdau mmoja hapo juu aliyesema anayo 33😂😂😂😂.
 
Back
Top Bottom