Hivi Azam mnapohamisha kuonyesha mechi kwenda ZBC AU Azam Extra huwa mnamtaarifu nani ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,788
218,420
Huwa nashangaa sana ninapoona mechi imetangazwa kuonyeshwa labda Azam Sports 2 , halafu muda unafika haionekani au imehamishiwa channel nyingine bila taarifa , hivi mnadhani ni nani ataota kwamba game hii iko channel ya ZBC 2 wakati mlitangaza kuwa itakuwa Azam Sports 3 ?

Kwa mfano , walitangaza kwamba game ya league 1 kati ya Rennes na Aj Auxerre ingeonyeshwa Azam Sports 3 , muda ulipofika game yenyewe hakuna Japo tangazo bado lipo , kumbe wameihamishia Azam Xtra ! sasa tutajuaje ? na hii si mara moja , huu ndio mchezo wao , hii kitu haikubaliki .

Badilikeni haraka sana , Ni kweli kwamba Azam ni yenu lakini sisi tunalipa hela zetu , msituburuze na tuheshimiane
 
Back
Top Bottom