Hivi, anachofanya Magufuli ni kampeni?

Hivi, anachofanya Magufuli ni kampeni?

Mnasihi

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2013
Posts
8,131
Reaction score
7,541
Ni jumapili iliyopita alikuwa uwanja wa Jamhuri Dodoma na jana Mwembeyanga Dar akinadi sera zake za "sitowaangusha". Msajili wa vyama pamoja na tume ya uchaguzi wamekaa kimya bila kusema lolote. Hii inamaanisha vyama vinaweza kuanza kampeni kabla tume ya uchaguzi haijaruhusu?
Au kwenu wadau limekaaje hili jambo? Tuelimishane wajuzi wa sheria na taratibu za uchaguzi bila kuingiza ushabiki na mihemko.
 
Anachofanya ni kampeni ya wazi: anazungumzia kuboresha maisha ya machinga na bodaboda.Kwa kuwa tume ya uchaguzi inapumulia kwenye mifuko ya suruwali za ccm, watamwacha aendelee kurutubisha matumaini ya wanaccm na mashabiki wao.
 
Kungekua na tume huru ya uchaguzi ingekua Technical knock out , nimemsikiliza leo asubuhi akihutubia huko mbagala na kila baada ya dakika mbili anasema hafanyi kampeni bali anajitambulisha.

Sifikirii kama kujitambulisha kunamruhusu kusema nini atakachokifanya pindi akichaguliwa.
 
Ni jumapili iliyopita alikuwa uwanja wa Jamhuri Dodoma na jana Mwembeyanga Dar akinadi sera zake za "sitowaangusha". Msajili wa vyama pamoja na tume ya uchaguzi wamekaa kimya bila kusema lolote. Hii inamaanisha vyama vinaweza kuanza kampeni kabla tume ya uchaguzi haijaruhusu?
Au kwenu wadau limekaaje hili jambo? Tuelimishane wajuzi wa sheria na taratibu za uchaguzi bila kuingiza ushabiki na mihemko.

mwembeyanga???? au viwanga vya Zakiem Mbagala
 
Na zile nyimbo zao za kampeni ndio kabisa, zile ni kampeni halisi.
 
Anachofanya ni kampeni ya wazi: anazungumzia kuboresha maisha ya machinga na bodaboda.Kwa kuwa tume ya uchaguzi inapumulia kwenye mifuko ya suruwali za ccm, watamwacha aendelee kurutubisha matumaini ya wanaccm na mashabiki wao.
Zingekuwa kampeni kama angefanya Mr, white hair, kwa vile ni wenyewe si kampeni.
 
Wanasheria wa vyama vya upinzani watadharaulika wakishindwa kufungua mashtaka ama kuweka pingamizi dhidi ya Dr. JPJ Magufuli.
 
Magufuli hafanyia kampeni bali anatambulishwa kwa wanachama wa CCM ambao ikitokea ameshinda na kuingia ikulu atakuwa akiwaongoza kama mwenyeti wao.
 
Hakuna cha kufungua mashtaka wala nini, kwani CCM wanaelewa wanachokifanya, hawaendi kinyume na taratibu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, hata Ukawa wakimpitisha mgombea wao ruksa kumtambulisha kwa wana chama wao.
 
Dawa na wao ukawa wazunguke nchi nzima kumtambulisha mgombea wao. Angalizo: Polisi wasije kusema intelligencia hairuhusu halafu mtiti ndio utaanzia hapo sasa!
 
Cha kufanya UKAWA wateue fasta mgombea, wajaze helicopter mafuta nae aanze kujitambulisha mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya na hata kata kwa kata...

Jino kwa jino hapa
 
Wanaoanza kampeni mapema wanakatwaga. Huyu atakatwa Oktoba. Acha arukeruke ila Oktoba ni mwendo wa baharini tu.
 
Anarudi kuwapa taarifa watanzania maana alipita kwao kuomba udhamini sasa anawapa mrejesho kuwa hawakufanya makosa kumdhamini na Oktoba ataapishwa uwanja wa UHURU hiyo siyo kampeni maana sijawaona makamanda kwenye msafara wake!Kampeni kuanza watatangaza Tume!
 
Magufuri alifaa akaanzishe band mana hana mvuto.

Ndugu acha kudharau fani za watu kuna watu wanasomesha watoto wao kwa kumiliki bendi, na tunauthamini sana mchango wa bendi za muziki hapa Tanzania vyama vyote vya siasa vinawategemea kwa nyimbo na burudani kwenye hamasa!Mimi siungi mkono maneno yako ya dharau kwa bendi za Muziki wa Tanzania eti tu mtu akiwa hana mvuto ndo akaanzishe bendi????wakati bendi ndiyo zinatumika kuwasafishia njia wagombea wenu!
 
Back
Top Bottom