Historia Ya Extra Musica (Sehemu ya II)

Uzi murua sana pamoja na mikwaruzano ya hapa na pale. Hii yote inaashiria mapenzi kwa mada iliyopo. Hongera mleta mada. Tafadhali sana lete historia ya wenge musica. Wale wapenzi wa bcbg big up mimi werason namkubali bhana. Meison mere chama la wananchi.
 
Dah..Extra Musica, Extraa Musica!!!!
Hii bendi enzi hizo ikiwa na wenyewe ndio nilikua naiona tamu sana, Ukitaka kuoa viwango vya akina Oxygene, Rousen, pappy bastin, DouDou na wengine cheki video ya Aigle Imperial. Hii Extra ya miaka hii kiukweli Roga Roga ameidominate sana..jamaa pekee anaenivutia sana ni Kassoumbalessa hasa kwenye Mogomboro na Gael Bitoma katupia sauti safi saana huyu.
 
Halafu mimi maisha yangu yote najua Roga Roga ni yule Jamaa mweupe, kumbe ni yule mwenye upara, Ameua sana kwenye OYO EKOYA EYA
 
Pamoja na kuheshim maelezo mazuri ya kundi la Extra Musica uliyayatoa, lakini kutaja jina la Jules Kibens kwenye wanamuzik wa Extra Musica lazima uweke maelezo vizuri, je hao wanamuziki wa Extra Musica alikutana nao Kinshansa au Brazzaville? Je huyo Jules Kibenga(Kibens) ni kutoka Congo RDC au Congo Republic?(Kinshasa au Brazzaville)
Naomba tu ufafanuzi.

Pia, katika lile kundi la Extra Musica International, nilikua naangalia nyimbo walizotoa, lakini kwenye orodha sikuona wimbo Mark 9:23(ule ambao video shooting mwishoni wanashuka kwenye helicopter)
 
Kikundi cha utamaduni( ukataja kikundi na mji) kisha ukamtaja muimbaji wa kundi hilo la utamaduni na mwenzie Jules Kibens, swali sasa

Hilo kundi lilikua nchi ya RDC/DRC au Congo Brazzaville, kwa maana ya mji ulioutaja uko nchi gani?
Kama ni Congo Brazzaville, je Jules Kibens alizaliwa na kukulia Congo Brazzavile na baadae kuhamia CONGO KINSHASA ambako baadae akajiunga na Wenge BCBG? Kuhusu Jules Kibens na uhusiano na Extra Musica ndugu Roga Roga naomba uniweke sawa, maana inacontradict kidogo!
 
Sehemu ile ya kwanza ulimyaja pia Jules Kibens kuwa nae ni mmoja wa waanzilishi wa Extra Musica, je ni kweli? Au uliweka kimakosa, kama ni kweli ni Mkongo Kishansa au Brazzavile?
huyu ni mkongo wa kin na sikumtaja kimakosa
 


huyu mzazi wake mmoja ni from brazaville, na walikuwa ni wanachama yeye, papy kakol na roga roga katika vikundi vya utamaduni enzi za ujana wao kabla wao (kibens na kakol ) kujiunga na kundi liitwalo patrouille des stars, kundi hili lilikuwa huko congo brazaville na wakati huo tulitegemea lingeleta upinzani wa juu kwa Extra Musica lakini haikuwa hivyo, kwani kiogozi wao (simkumbuki jina ) alifariki miaka ya 90 (kama sijakosea ni 19996) na wao (kakol na Kibens) kuhamia kinshasa na huo ukawa mwisho wa kundi hili la patrouille des stars na mwanzo mpya wa kibens na kakol kinshasa. Bonyeza link hiyo uone moja ya nyimbo za kundi la patrouille des stars (kibens na kakol wakiwa brazaville)
Okala
 
Nilikuwa nampenda sana rogatien kumbe alivyo sivyo nilivyomdhania.
 
Mkuu CHAZA nitashukuru ukini wekea audio za Wenge BCBG Album ya kalaye boinge & Pentagon [emoji120][emoji120]
 
Mkuu CHAZA nitashukuru ukini wekea audio za Wenge BCBG Album ya kalaye boinge & Pentagon [emoji120][emoji120]
Pentagon ninazo No Comment Shenghen pamoja na Filandu. Jinsi ya kuziweka sina uhakika sana
 
Aiseee,ahsante sana kwa haya madini. Barikiwa sana. Ipo nadharia kuwa kundi la G7 liliasisiwa kuliua kundi la Extra Musica na hata Wenge,ilikuaje lilisambaratika ghafla? Kiukweli walileta ngoma kali sana kwenye Album yao mpya ya Ca aver(spelling error)!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…